Vikosi vya Msaada wa Haraka, RSF, vinahusika katika mapigano na Wasudan wakiongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, makamu mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Uhuru wa Sudan, anajulikana kama 'Hemedti'.
Kikosi hiki cha kijeshi, ambacho kina makao makuu kote nchini, kina wapiganaji wapatao 100,000.
RSF ilitokana na kundi la wanamgambo wa Janjaweed lililotumiwa na Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir dhidi ya waasi katika eneo la Darfur katika miaka ya 2000.
Baada ya muda, RSF imepanuka na kutumika kama walinzi wa mpaka, hasa kupambana na uhamiaji usio wa kawaida.
Kuanzia mwaka 2015, RSF ilianza kutuma wanajeshi kupigana pamoja na jeshi la Sudan katika vita vya Yemen, pamoja na wale wa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, kuimarisha uhusiano wa Dagalo na Mataifa ya Ghuba.
Mnamo mwaka wa 2017, sheria ilipitishwa kuhalalisha kundi hilo kama jeshi huru la usalama.
Kuhusika katika mapinduzi Mnamo Aprili 2019, RSF ilishiriki katika mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa Omar al-Bashir mamlakani.
Mwanauchumi mashuhuri
Abdalla Hamdok aliapishwa kama waziri mkuu wa Sudan na kiongozi wa baraza la mawaziri la mpito kufuatia mapinduzi hayo.
Baadaye mwaka huo huo, Jenerali Dagalo alitia saini makubaliano ya kugawana madaraka ambayo yalimfanya kuwa naibu wa baraza tawala la kijeshi linaloongozwa na jenerali wa jeshi Abdel Fattah al Burhan.
Kabla ya mkataba huo kutiwa saini mwaka 2019, wanaharakati walishutumu kundi la wanamgambo kwa kuhusika katika mauaji ya waandamanaji wengi wanaounga mkono demokrasia.
Mashirika ya haki za binadamu pia yaliwashutumu wapiganaji wa RSF kwa ghasia za kikabila.
Jenerali Dagalu ameondoa kinga ya baadhi ya watu wake, na kuruhusu wahukumiwe. Aliomba radhi mwaka jana kwa uhalifu uliofanywa na serikali dhidi ya watu wa Sudan.
RSF pamoja na jeshi walishiriki tena katika mapinduzi ambayo yalikatiza mpito kwa utawala wa kiraia na uchaguzi uliopangwa mapema Oktoba 2021 ambao haukufanyika.
Kufuatia mapinduzi hayo, Jenerali wa jeshi al Burhan alikua mkuu wa nchi huku Hamdan Daglo akiwa naibu wake.
Lakini mkuu wa RSF Hamdan Dagalo tangu wakati huo amejitenga na mapinduzi ya 2021 akielezea kama ''kosa'' kauli ambayo iliashiria mpasuko wa kwanza wa wazi na jenera al Burhan.
Mvutano wa hivi karibuni
Jeshi Chini ya shinikizo kubwa la kimataifa na kikanda, vikosi vya jeshi na RSF vilitia saini makubaliano ya awali mwezi Desemba mwaka jana na makundi yanayounga mkono demokrasia na kiraia - yenye lengo la kuirejesha nchi kwenye demokrasia
Lakini makubaliano yaliyoratibiwa kimataifa yalitoa muhtasari mpana tu, na kuacha masuala ya kisiasa yenye miiba migumu zaidi kutotatuliwa
Wakati wa mazungumzo magumu kufikia makubaliano ya mwisho, mvutano kati ya Jenerali wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa nchi na naibu wake Hamdan Dagalo uliongezeka
Mzozo muhimu ulikuwa juu ya jinsi RSF ingejumuishwa katika jeshi la kawaida na nani angekuwa na udhibiti wa mwisho juu ya wapiganaji na silaha.