| Swahili
AFRIKA
1 DK KUSOMA
Uganda:Mtumiaji wa TikTok ashitakiwa kwa kumtukana Rais Museveni
Mtengeneza maudhui huyo, Emmanuel Nabugodi amekiri kosa lake huku waendesha mashitaka wakitaka apewe adhabu ya miaka saba jela.
Uganda:Mtumiaji wa TikTok ashitakiwa kwa kumtukana Rais Museveni
Rais Yoweri Museveni wa Uganda./Picha: Reuters / Others
14 Novemba 2024

Mtengeneza maudhui wa Uganda, Emmanuel Nabugodi anakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela kwa kumdhihaki Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni.

Mtengeneza maudhui huyo, anashitakiwa kwa kosa la kuchapisha picha mjongeo kwenye mtandao wa TikTok, yenye ujumbe wa kuchapwa viboko hadharani kwa Rais Museveni, mwendesha mashitaka wa umma alisema siku ya Alhamisi.

Nabugodi alikiri kosa lake na anatarajiwa kuhukumiwa siku ya Novemba 18, 2024.

Mwanasheria wa Serikali Paul Aheebwa Byamukama amesema kuwa waendesha mashitaka wameitaka mahakama hiyo ya Entebbe kumpa mshitakiwa huyo kifungo cha miaka saba gerezani.

Nabugodi anakuwa mganda wa nne kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumtukana Rais wa nchi hiyo na familia yake.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika