| Swahili
MICHEZO
2 DK KUSOMA
Droo Kombe la mataifa bora Ulaya UEFA EURO 2024 kufanyika Jumamosi, Desemba 2
Wenyeji Ujerumani walifuzu moja kwa moja pamoja na timu nyingine 20 zimefuzu moja kwa moja na kujihakikishia nafasi zao kwenye fainali hizo
Droo Kombe la mataifa bora Ulaya UEFA EURO 2024 kufanyika Jumamosi, Desemba 2
Droo ya Kombe la EURO 2024 kufanyika Disemba 2 / Others
1 Desemba 2023

Droo ya UEFA Euro 2024 itafanyika rasmi Jumamosi tarehe 2 Desemba huku timu 23 zikijiunga na Wenyeji Ujerumani katika fainali za msimu ujao wa joto.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Ujerumani kuandaa mashindano ya Uropa ya UEFA tangu pande za Ujerumani kuungana tena.

Jiji la Hamburg la Ujerumani, mojawapo ya miji 10 itakayoandaa ngarambe za EURO 2024, litakuwa mwenyeji wa droo ya siku ya Jumamosi ambayo itaanza saa mbili usiku.

Italia ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo la Ulaya, kwani walishinda taji la EURO 2020.

Ujerumani na Uhispania ndio wamiliki wa rekodi ya mataji mengi ya EURO, wakiwa na mataji matatu kila mmoja.

Vyungu kuelekea droo

  • Chungu Cha 1: Ujerumani (nchi mwenyeji), Ureno, Ufaransa, Hispania, Ubelgiji, Uingereza

  • Chungu Cha 2: Hungaria, Uturuki, Romania, Denmark, Albania, na Austria

  • Chungu Cha 3: Uholanzi, Scotland, Kroatia, Slovenia, Slovakia, Jamhuri ya Cheki

  • Chungu Cha 4: Italia, Serbia, Uswisi, mshindi wa mechi za mtoano A, mshindi wa mechi za mtoano B, mshindi wa mechi za mtoano C

CHANZO:TRT Afrika