| Swahili
MICHEZO
2 DK KUSOMA
EURO 2024: Uingereza kukutana na Uswisi kwenye robo fainali
Slovakia ilitangulia katika mchezo huo kufuatia bao la dakika ya 25 lililofungwa na Ivan Schranz na baadaye nahodha Hary Kane kuihakikishia Uingereza nafasi ya kucheza Robo Fainali.
EURO 2024: Uingereza kukutana na Uswisi kwenye robo fainali
Jude Bellingham akifunga bao la kusawazisha dhidi ya Slovakia, Juni 30, 2024./Picha: Reuters / Others

Timu ya taifa ya Uingereza imetinga hatua ya Robo Fainali ya michuano ya EURO 2024, yanayoendelea nchini Ujerumani baada ya kuifunga Slovakia 2-1.

Hata hivyo, iliwalazimu Uingereza isubirie dakika za mwisho za muda wa nyongeza katika kipindi cha pili, ili izawazishe bao lililofungwa na Jude Bellingham.

Awali, Uingereza walidhani kuwa wamerudisha goli katika dakika ya 50 kupitia kwa Phil Foden, lakini mwamuzi wa mchezo huo alikata bao hilo kwani kiungo huyo alikuwa ameotea.

Slovakia ilitangulia katika mchezo huo kufuatia bao la dakika ya 25 lililofungwa na Ivan Schranz na baadaye nahodha Hary Kane kuihakikishia Uingereza nafasi ya kucheza Robo Fainali.

Uingereza itakutana na Uswisi katika mchezo wao Robo Fainali Julai 6, 2024.

Ikumbukwe kuwa, Uingereza ilifika hatua ya fainali ya michuano ya EURO 2020 yaliyofanyika nchini Uingereza, baada ya kufungwa na Italia.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika