Wanariadha hao walichaguliwa na jopo la kimataifa la wataalam wa riadha, linalojumuisha wawakilishi kutoka maeneo yote sita ya bara ya riadha ulimwenguni.
Mchakato wa upigaji kura kwa wanariadha bora wa dunia wa mwaka wa 2023 umefunguliwa wiki hii kabla ya tuzo za riadha duniani 2023.
Tigist Assefa, Ethiopia, Mbio za Marathon
Mshindi wa mbio za marathon za Berlin
Rekodi ya dunia ya marathon
Femke Bol, Uholanzi, 400m/400m kuruka Vihunzi
Bingwa wa dunia mbio za 400m kuruka vihunzi
Ameweka rekodi ya dunia ya ndani ya mita 400
Shericka Jackson, Jamaika, 100m/200m
Bingwa wa dunia wa mita 200 na mshindi wa medali ya fedha ya mita 100
Bingwa wa mbio za ligi ya Diamond 100m na 200m
Faith Kipyegon, KEN, 1500m/mile/5000m
Mshindi wa mbio za 1500m and 5000m duniani
Ameweka rekodi mpya katika mbio za 1500m, maili na 5000m
Haruka Kitaguchi, Japani, mrushaji mkuki
Bingwa wa dunia
Bingwa wa ligi ya Diamond
Yaroslava Mahuchikh, Ukraine, mruka juu
Bingwa wa dunia
Bingwa wa ligi ya Diamond
Maria Perez, Uhispania, mbio kutembea
Bingwa wa dunia 20km na 35km mbio za kutembea
Anashikilia rekodi ya dunia katika 35km mbio kutembea
Gudaf Tsegay, Ethiopia, 5000m/10,000 m
Mshindi wa dunia wa mita 10,000
Mshindi wa ligi ya Diamond mbio za 5000m na ameweka rekodi ya dunia
Sha'carri Richardson, 100m/200m
Bingwa wa dunia katika mbio za mita 100
Mshindi wa medali ya shaba duniani katika mbio za mita 200
Yulimar Rojas, Venezuela kuruka mara tatu
Bingwa wa dunia
Bingwa wa ligi ya Diamond
Winfed Yavi, Bahrain, 3000m kuruka vihunzi na maji
Mshindi wa Dunia
Bingwa wa ligi ya Diamond na muda unaoongoza duniani
Shughuli ya upigaji kura kumchagua mwanariadha bora wa dunia wa mwaka itafungwa saa sita usiku, ifikapo Jumamosi Oktoba 28.
Mchakato huo wa kupiga kura utafuatwa na tangazo la wanawake watano na wanaume watano bora wa mwisho litakalofanywa shirikisho la riadha dunini tarehe 13-14 Novemba.
Washindi wa mwanariadha bora wa kike na wa kiume watatangzwa rasmi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii ya shirikisho la riadha duniani World Athletics tarehe 11 Desemba.












