| Swahili
MICHEZO
1 DK KUSOMA
Kevin-Prince Boateng wa Ghana atangaza kustaafu
Boateng alichagua kuichezea Ghana katika ngazi ya kimataifa mwaka 2010 licha ya kuiwakilisha Ujerumani katika ngazi ya vijana.
Kevin-Prince Boateng wa Ghana atangaza kustaafu
Boateng: Klabu yake ya mwisho ilikuwa Hertha Berlin ya Ujerumani ambapo alianza uchezaji wake wa soka. Picha: GETTY / Others
13 Agosti 2023

Kiungo wa zamani wa Ghana Kevin-Prince Boateng ametangaza rasmi kustaafu soka ya kulipwa akiwa na umri wa miaka 36.

Mchezaji huyo mzaliwa wa Berlin, alikuwa na safari ya kuviwakilisha vilabu mbalimbali barani Ulaya, ambapo aliichezea Ujerumani, Uingereza, Uturuki, Uhispania na Italia.

Miongoni mwa timu alizowakilisha katika vilabu 15 ni Mabingwa wa Uhispania Barcelona, Mababe wa Italia AC Milan, Fiorentina, Besiktas, na Hertha Berlin.

Kimataifa, aliiwakilisha Ghana, na kucheza kwenye Kombe la Dunia 2010 na 2014. Kwa jumla, alipiga mechi 15 kwa Black Stars, huku akifunga mabao mawili, huku kustaafu kwake kukifungia pazia la taaluma yake ya kipaji cha hali ya juu.

CHANZO:TRT Afrika