Msimu wa Ligi ya Mabingwa Uefa Champions League kuanza/ Picha: UEFA

Hatimaye baada ya pumziko lililofuata ubingwa wa Manchester City wa taji la Uefa Champions League msimu uliopita, safari ya kulitwaa taji hilo limeanza tena kwa vilabu vya ulaya huku jumla ya timu 16 zikishuka dimbani leo, wakati jumla ya mechi nane zikiwa zimeratibiwa.

Manchester City, waliweka historia msimu uliopita kwa kuwa mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya kuishinda Inter Milan katika fainali iliyochezeshwa katika Uwanja wa Olimpiki wa Ataturk, Istanbul.

City itacheza dhidi ya timu kutoka Serbia kwa mara ya kwanza ikiialika Crvena Zvezda, ambao wanaoshiriki hatua ya makundi, kwa mara yake ya tatu.

Mchezaji bora wa UEFA Mwaka huu, Erling Haaland wa Manchester City. Picha: Getty.

Newcastle United ya Uingereza, inarejea ligi ya klabu bingwa baada ya kutokuwepo kwa miaka 11, kwenye mashindano hayo tangu 2002/03 na watafungua kampeni yao dhidi ya jitu lingine la bara, mabingwa wa Uropa Mara saba, Milan, ugenini.

Borussia Dortmund watasafiri hadi mji mkuu wa Ufaransa wa Paris kuwinda pointi tatu watakapokabiliana na Paris Saint-Germain katika mechi ya kundi hili la Kifo la 'F' ambalo linatarajiwa kuwa gumu kwani pia lina AC Milan ya Italia na Newcastle United.

Mabingwa wa ligi kuu ya Scotland Celtic wataanza kampeni yao ya Kundi E Rotterdam dhidi ya wamiliki wa taji la Eredivisie, Feyenoord ya Uholanzi jioni hii.

FC Barcelona itacheza dhidi ya Klabu ya Ubelgiji ya Royal Antwerp.

Antwerp inafunzwa na kiungo wa zamani wa Barcelona Mark van Bommel, ambaye alishinda tuzo huyo na mahispania hao akicheza pamoja nao na kocha wa sasa Xavi Hernández mwaka 2006.

Fainali za msimu huu wa ligi hiyo ya mabingwa ya UEFA utahitimishwa katika Uwanja wa Wembley jijini London nchini Uingereza.

  • AC Milan vs Newcastle (Mechi ya Kundi F)
  • Young Boys vs Leipzig (Mechi ya Kundi G)
  • Feyenoord vs Celtic (Mechi ya Kundi E)
  • Lazio vs Atlético de Madrid (Mechi ya Kundi E)
  • Paris vs Dortmund (Mechi ya Kundi F)
  • Man City vs Crvena zvezda (Mechi ya Kundi G)
  • Barcelona vs Antwerp (Mechi ya Kundi H)
  • Shakhtar Donetsk vs Porto (Mechi ya Kundi H)

Mechi nyingine itakuwa kati ya Shakhtar ya Ukraine na miamba wa Ureno, Porto. Shakhtar wanajiandaa kuingia ngarambe za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa vishindo huu ukiwa msimu wao wa 18 katika mashindano hayo.

TRT Afrika