Tanzania: Karibia kikosi kizima cha Afcon 2023 chaachwa nje ya timu ya taifa ya Soka, Taifa Stars

Tanzania: Karibia kikosi kizima cha Afcon 2023 chaachwa nje ya timu ya taifa ya Soka, Taifa Stars

Nyota wa KRC Genk Kelvin John miongoni mwa mastaa wapya waliopewa namba katika kikosi cha Taifa Stars katika mechi za kirafiki Saudi Arabia
Kikosi cha awali cha timu ya  taifa ya SokaTanzania, Taifa Stars kwenye Afcon 2023. Picha: TFF

Kaimu kocha wa timu ya taifa ya mpira wa miguu Tanzania Hemedi Suleiman ‘Morocco,’ amechagua kikosi cha wachezaji 21 kitakachochuana na Sudan nchini Saudi Arabia kwa kutoa fursa kwa wachezaji chipukizi.

Aidha, karibia kikosi kizima cha Afcon 2023 kimeachwa nje ya timu ya timu hiyo ya Taifa Stars huku baadhi tu ya walioshiriki Dimba hilo akiwemo Ben Anthony Starkie (Ilkeston-England), Tarryn Allarakhia (Wealdstone – England) na Mohammed Ali Omar Sagaf (Boreham Wood – England), wakidumishwa kikosini.

Wachezaji hao waliotajwa, ambao wengi wakiwa ni vijana na chipukizi, wamepewa fursa na Kocha Hemedi Suleiman 'Morocco,' ambaye alichukua nafasi hiyo ndani ya Kombe la Afcon, na ana matumaini waterejesha imani yake kwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao mbili za kirafiki dhidi ya Sudan nchini Saudi Arabia.

Makipa: Ahmed Ali Suleiman (Uhamiaji FC), Ally Salum Juma (Simba SC), Na Abraham Vuai Nassoro (Azam FC (FIFA TDS).

Walinzi: Abdulmalik Adam Zakaria (Namungo FC), Baraka Shabaan Mtuwi (Mashujaa FC), Abdulrahim Seif Bausi, (Uhamiaji FC, Mukrim Issa Abdallah (Hefu FC), Alphonce Mabula Msanga (Rfk Novi Sad, Serbia), Miano Danilo Van den Bos - Alicante, (Uhispania), na Gadiel Michael Kamagi anayewakilisha Cape Town Spurs, Afrika Kusini.

Viungo: Mohammed Ali Omar Sagaf (Boreham Wood – England), Morice Michael Abraham (RFK Novi Sad – Serbia), Khalid Habib Idd (Singida FC), Ishaka Saidi Mwinyi (KMK FC) na Jabir Seif Mpanda , Getafe, Uhispania.

Washambuliaji: Omary Abdallah Omary (Mashujaa FC), Ben Anthony Starkie (Ilkeston – England), Oscar Adam Paul (Kakamega FC – Kenya), Kelvin Pius John (KRC Genk – Ubelgiji), Tarryn Allarakhia (Wealdstone – England) na Ibrahim Hamad Ahmada (Zimamoto FC).

TRT Afrika na mashirika ya habari