| Swahili
UTURUKI
2 DK KUSOMA
Jukwaa la TRT World kuangazia changamoto za ulimwengu
Zaidi ya wazungumzaji 150 kutoka nchi zaidi ya 30 watashiriki katika jukwaa hilo ambalo Rais Erdoğan atatoa hutoba ya ufunguzi.
Jukwaa la TRT World kuangazia changamoto za ulimwengu
Jukwaa  la mwaka huu litahusisha mijadala mbalimbali yahusuyo Mashariki ya Kati, Gaza, Uturuki, Afrika na mgogoro kati ya Urusi na Ukraine./Picha: TRT World / Others
21 Novemba 2024

Jukwaa la nane la TRT World linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 hadi 30 Novemba, likiwaleta pamoja wazungumzaji zaidi ya 150 kutoka nchi zaidi ya 30 kujadiliana changamoto mbalimbali ulimwenguni.

Likiwa limeandaliwa na Shirika la Habari la TRT, jukwaa hilo litafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Istanbul.

Jukwaa hilo, limewahi kuwaleta pamoja maelfu ya wageni na wazungumzaji 767.

Kwa mwaka huu, jukwaa hilo litaangazia mijadala mbalimbali ikiwemo suala la Mashariki ya Kati na Gaza, Uturuki, Afrika, mgogoro wa Urusi na Ukraine, mabadiliko ya tabia nchi, vita, teknolojia, vyombo vya habari, sheria za kimataifa na uchumi.

Rais wa Uturuki, ambaye amehudhuria majukwaa hayo mara kwa mara toka mwaka 2017, anategemewa kuhutubia jukwaa hilo, akiangazia masuala mbalimbali ulimwenguni.

Dondoo muhimu zaidi za mkutano huo zinapatikana kupitia : www.trtworldforum.com.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika