| Swahili
UTURUKI
1 DK KUSOMA
Uturuki kuendelea kuweka wazi yanayoendelea Gaza, Rais Erdogan
Kulingana na Erdogan, upinzani wa siku 471 uliofanywa na Hamas, ni dhihirisho tosha la kutokukata tamaa.
Uturuki kuendelea kuweka wazi yanayoendelea Gaza, Rais Erdogan
Siku ya Jumatano, Rais Erdogan alikutana na ujumbe wa Hamas jijini Ankara, akiwemo mkuu wa Baraza la Shura ya Hamas Muhammad Darwish, katika jengo la Ikulu./Picha: AA / Others
29 Januari 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, itaendelea kuanika yanayoendelea Gaza, akionesha matumaini ya kukamilika kwa awamu tatu za usitishwaji wa mapigano.

Siku ya Jumatano, Rais Erdogan alikutana na ujumbe wa Hamas jijini Ankara, akiwemo mkuu wa Baraza la Shura ya Hamas Muhammad Darwish, katika jengo la Ikulu.

Kulingana na Erdogan, upinzani wa siku 471 uliofanywa na Hamas, ni dhihirisho tosha la kutokukata tamaa.

Rais Erdogan alisisitiza kuwa Uturuki itaendelea kuzungumzia ukweli wa yanayoendelea Gaza pamoja na kuendelea kuipa misaada.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na maofisa wa ngazi ya juu wa Uturuki, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Mkuu wa Idara ya Intelijensia ya Taifa (MIT) Ibrahim Kalin, na Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika