| Swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Blinken aitetea kura turufu ya Marekani, huku miili zaidi ya 40 ikikusanywa
Mashambulizi ya Israel dhidi ya mji wa Gaza, yameingia siku ya 140 na kushuhudia vifo vya wapalestina 29,410, wengi wao wakiwa ni watoto na kujeruhi wengine 69,465.
Blinken aitetea kura turufu ya Marekani, huku miili zaidi ya 40 ikikusanywa
Wapalestina wengi, wakiwemo watoto wanapelekwa katika hospitali ya mashahidi wa Al Aqsa kwa ajili ya matibabu kufuatia mfululizo wa mashambulizi kutoka majeshi ya Israel./Picha: AA   / Others
23 Februari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amejibu tuhuma ya nchi yake kujitenga katika mchakato wa kutafuta suluhu ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina, akisema, "Sote tuna malengo yanayofanana."

"Kila mtu angependa kuona vita hivyo vikikoma haraka iwezekanavyo," alisema Blinken katika mkutano na waandishi wa habari nchini Brazil, wakati anajibu tuhuma ya Marekani kujitenga, na namna inavyoiunga mkono Israel na namna inavyotumia kura yake ya turufu dhidi ya azimio la Umoja wa Mataifa wa kumaliza vita hivyo.

"Nadhani wote tumeungana katika jukumu hili la kutaka kuona amani ya kweli na endelevu," alisema.

"Hili azimio peke yake haliwezi kusitisha mapigano hayo. Swali lililo mbele yetu ni namna gani tutawaokoa mateka, kuongeza misaada ya kibinadamu na hatimaye kumaliza mapigano hayo," alisema Blinken katika maelezo yake kuhusu kura ya turufu ya Marekani.

CHANZO:TRT Afrika