MICHEZO
1 dk kusoma
Wanariadha wa Kenya washinda mbio za marathon za New York kwa wanaume na wanawake
Kenya iliwakilisha vyema kwa mbio za Marathon za New York Jumapili, wakati Benson Kipruto alipomaliza kwa muda wa saa mbili dakika nane na sekunde tisa kwa wanaume huku Hellen Obiri akiweka rekodi ya New York kwa wanawake katika muda wa 2:19:51.
Wanariadha wa Kenya washinda mbio za marathon za New York kwa wanaume na wanawake
Mwanariadha wa Kenya Hellen Obiri ameshinda marathon ya New York kwa wanawake Novemba 2, 2025. / Picha:AP
3 Novemba 2025

Kenya iliwakilishwa vyema kwenye majukwaa ya wanaume na wanawake katika mbio za Marathon za jiji la New York City siku ya Jumapili, wakati Benson Kipruto alipomaliza mbio hizo katika muda wa saa mbili dakika nane na sekunde tisa naye Hellen Obiri akishinda upande wa wanawaeke na kuweka rekodi mpya ya mbio za jiji hilo katika muda wa 2:19:51.

Kipruto alikimbia kwa kasi zaidi hatua ya mita 50 za mwisho akimzuia Alexander Mutiso, ambaye alikuwa anapambania kukata utepe, Mutiso alimaliza wa pili kwa karibu sana, naye mshindi wa 2021 Albert Korir akimaliza wa tatu (2:08:57).

Mshindi wa medali ya shaba wa Paris Obiri, ambaye alishinda 2023, aikuwa anapambana sako kwa bako na Sharon Lokedi aliyemaliza wa pili katika muda 2:20:07, kabla ya kuamua kwenda kasi na kuvunja rekodi ya marathon hiyo kwa wanawake iliyowekwa na Margaret Okayo miaka 22 iliopita ya muda wa 2:22:31.

Bingwa wa mwaka jana Sheila Chepkirui (2:20:24) alimaliza wa tatu.