tokea masaa 2
Serikali ya Malawi imepiga marufuku usafirishaji nje wa mazao kwa lengo la kukuza usalama wa chakula nchini humo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchini Malawi Charity Musonzo alisema kuwa mpango huwa unalenga la kuhuisha usambazaji wa chakula, kudhibiti bei za mazao ya chakula na kulinda uhai wa wananchi wa Malawi wenye kutegema mahindi kama zao lao la chakula.
“Zao la mahindi lipo chini Sheria ya Udhibiti wa mazao, hivyo ni makosa kusafirisha bila ruhusa maalumu,” alisema Musonzo.
Malawi inakabaliana na uhaba mkubwa wa chakula ambao umeathiri takribani watu milioni 4.
Wakati ufunguzi wa mwaka wa bajeti kwa mwaka 2025, Rais Arthur Peter Mutharika aliielezea hali hiyo kama janga la kitaifa akiitaka jumuiya ya kimataifa kutoa msaada.













