| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Trump asema Marekani 'lazima iichukue' Greenland, huku akipendekeza mazungumzo
Rais wa Marekani anasema majadiliano kuhusu Greenland yatafanyika na viongozi mbalimbali wanaoshiriki Jukwaa la Uchumi wa Dunia, ambalo lilianza Jumatatu.
Trump asema Marekani 'lazima iichukue' Greenland, huku akipendekeza mazungumzo
Rais Donald Trump alipozungumza na waandishi wa habari kabla ya kupanda Air Force One katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Palm Beach. / AP
20 Januari 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Denmark haina uwezo wa kutosha wa kuilinda, akiashiria kwamba, sakata hilo litajadiliwa na viongozi wa dunia katika Jukwaa la Uchumi wa Dunia huko Davos.

"Sidhani kama watakataa," Trump aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu alipoombwa kutoa kauli yake kwa viongozi wa Ulaya wanaokutana Davos.

"Angalia, lazima tuipate. Hili lazima lifanyike. Hawawezi kuilinda, Denmark, ni watu wazuri," aliongeza.

Huku akiisifu Denmark na uongozi wake, Trump alisema, “Najua viongozi ni watu wazuri, lakini hata hawaendi huko."

Rais huyo wa Marekani amesema majadiliano ya Greenland yatafanyika na viongozi mbalimbali wanaohudhuria Jukwaa la Uchumi wa Dunia, ambalo limeanza Jumatatu.

“Tutalizungumza na watu mbalimbali," amesema, bila kutaja ni viongozi gani.

Greenland ni "muhimu sana," alisisitiza.

Rais amezungumzia kuhusu wasiwasi wa muda mrefu wa kiusalama, na kusema NATO imeitahadharisha Denmark kwa miongo kadhaa kuhusu tishio la kiusalama katika kanda.

“NATO imeitahadharisha Denmark kwa takriban miaka 20 sasa-zaidi ya hiyo 25," Trump amesema.

Ameelezea wasiwasi wake kwa Urusi, na kuongeza kuwa China pia ni tishio katika eneo la Arctic.

"Kwa hiyo tutaona kitakachotokea. Lakini tuseme hivi, utakuwa mkutano uliochangamka Davos," amesema.