UTURUKI
1 dk kusoma
Kauli maarufu za Erdogan zarindima jijini New York
Rais arudia wito wake wa mabadiliko kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akisema: “Ulimwengu ni mkubwa kuliko nchi tano.”
Kauli maarufu za Erdogan zarindima jijini New York
Ujumbe wa Erdogan wavuma jijini New York wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. / AA
24 Septemba 2025

Picha ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, pamoja na kauli zake maarufu “Ulimwengu ni mkubwa kuliko nchi tano” na “Ulimwengu wa haki zaidi unawezekana” ziliwekwa kwenye barabara kuu na mitaa ya kati jijini New York.

Hizi ni kauli ambazo Erdogan amekuwa akizirudia kwa muda mrefu akitaka mabadiliko katika mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Kwa miaka mingi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekosolewa kwa madai kuwa wanachama wake watano wenye kura ya turufu – Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China – wana ushawishi mkubwa usio wa haki.

Akihutubia kikao cha 80 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne, Erdogan alisisitiza tena wito wake wa kutaka mabadiliko ndani ya Umoja huo.

“Ulimwengu wa haki zaidi unawezekana”

“Ninaamini kwa dhati kwamba ni jukumu letu sote kuchukua hatua zitakazoirudisha Umoja wa Mataifa kwenye misingi yake ya awali katika mwaka huu wa 80 tangu kuanzishwa kwake.

“Tutaendelea kusema, ‘Ulimwengu ni mkubwa kuliko nchi tano!’ hadi pale mfumo wa haki, na si wa nguvu pekee, utakapowekwa,” alisema.

Kauli yake “Ulimwengu wa haki zaidi unawezekana” pia ilionyeshwa kwenye skrini za LED katika eneo la Times Square jijini New York.

CHANZO:TRT World