Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ametia saini azimio la pamoja la kuzuia watoto wa Gaza kutokupata haki yao ya elimu, wakati mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina yakiendelea.
Emine Erdogan alimbatana na Rais Recep Tayyip kwenye mkutano wa pamoja wa Umoja wa Nchi za Kiislamu na Jumuiya za Kiarabu, uliofanyika Doha nchini Qatar na kukutana na Sheikha Moza bint Nasser, ambaye ni mama mzazi wa kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani.
Taarifa ya pamoja iitwayo “Mwaka mbaya kwa wanafunzi waishio sehemu za migogoro” iliandaliwa na taasisi ya Education Above All Foundation.
Azimio hilo limetaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka za kumalizwa kwa ukiukwaji wa haki za watoto na mifumo ya elimu huko Gaza.
“Mbali na hayo, mauaji ya kimbari ya Gaza yanayofanywa na Israel yanasababisha ‘mauaji ya elimu’, na uharibifu wa mifumo ya elimu,” azimio hilo lilisema.
"Leo tunaungana kumaliza mauaji haya na tunaahidi kufanya kazi pamoja kutoa fursa za elimu na kuwasaidia watoto wapone," ilisema taarifa hiyo.
Azimio hilo, pia lilitiwa saini na balozi wa hiari wa UNESCO, akiwemo pia mke wa Rais wa Malaysia.