UTURUKI
2 dk kusoma
Tamthilia ya Kituruki ‘Teskilat’ inaangazia idadi ya raia waliouawa katika vita vya Gaza
Tamthilia ya Teskilat inaangazia madhara kwa raia katika mgogoro wa Gaza, ikionesha hospitali ziloshambuliwa kwa mabomu, njaa kutumika kama silaha, na ukosefu wa uwajibikaji katika vita kwenye msimu mpya wa tamthilia hiyo.
Tamthilia ya Kituruki ‘Teskilat’ inaangazia idadi ya raia waliouawa katika vita vya Gaza
tokea masaa 2

Tamthilia maarufu ya TRT Teskilat imeangazia athari za vita vya Gaza kwa watu katika msimu wake mpya, ikitumia mazungumzo makali kuangazia matatizo ya raia.

Katika sehemu moja ya hivi karibuni, waigizaji wakuu wanajadili athari za mashambulizi ya kijeshi, wakiashiria “kushambuliwa kwa mabomu kwa hospitali na kambi” na kueleza “njaa” kutumiwa kama “silaha mpya.” 

Mazungumzo pia yanaibua neno “mauaji ya halaiki” katika masuala yanayohusu Gaza.

Muigizaji mmoja anaonya, “Hatua zetu ni za kijasiri,” tukiangazia mauaji ya raia na uharibifu, huku mwingine akijibu, “Tuko kwenye vita na hatuwezi kukata tamaa,” akisisitiza mvutano kati ya malengo ya kijeshi na hofu kuhusu hali za watu. 

‘Wakati mmoja wakiwa wameathiriwa na mauaji ya halaiki, sasa wanauwa watu wasio na hatia Gaza’

Suala lingine wanaangazia ni mtazamo wa kimataifa, huku muigizaji mmoja akieleza kuwa taifa lao, “ambalo wakati mmoja liliathiriwa na mauaji ya halaiki,” sasa linaonekana “likiwaua watu wasiokuwa na hatia Gaza,” ambapo mwenzake anasisitiza kuwa ‘’hizo ardhi ni zetu” na kutaka waendelee kufanya hivyo.

Watayarishaji wamesambaza sehemu ndogo ya tamthilia hiyo, ambayo inaonesha maigizo kuhusu suala la kulinda raia, usawa, na sheria za vita. 

Kuwepo kwa mazungumzo kama hayo wakati ambapo watu wengi wanatizama, Teskilat inaangazia majadiliano yanayoendelea miongoni mwa wanadiplomasia, mashirika ya haki za binadamu, na vyombo vya habari kuhusu uwajibikaji, kutoa misaada kwa watu, na changamoto za maadili katika mapigano ya kisasa.

Tamthilia inayoangazia uhalisia kama ulivyo

Israel inaendelea kuwaua raia huko Gaza—zaidi ya nusu yao wakiwa watoto —huku mataifa ya Magharibi yakielekea kutambua Palestina na jamii ya kimataifa ikishtumu matumizi ya njaa kama silaha.

Mwezi Agosti, Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa Gaza itakuwa na baa baya la njaa kuwahi kutokea. Mashirika ya misaada ya kimataifa yameonya kuwepo kwa njaa mbaya zaidi katika eneo lote.

Wizara ya Afya ya Gaza imeorodhesha kuwepo kwa vifo visivyopunguwa 440 kutokana na njaa na utapiamlo,nusu yao wakiwemo watoto.

Zaidi ya Wapalestina 2,000 wameuawa wakijaribu kufikia malori ya misaada ya chakula au wakisubiri misaada katika vituo vya usambazaji.

CHANZO:TRT World