| Swahili
ULIMWENGU
6 DK KUSOMA
Israeli yaharibu viinitete 5000 vya IVF mjini Gaza
Shambulio la Israel katika kituo cha Al Basma IVF mjini Gaza, mwezi Disemba, umeua matumaini ya mwisho kwa mamia ya wanandoa wa Kipalestina wanaokabiliwa na utasa
Israeli yaharibu viinitete 5000 vya IVF mjini Gaza
Kituo cha Al Basma IVF mjini Gaza chashambuliwa na Israeli. Picha: Reuters / Others
18 Aprili 2024

Wakati kombora la Israel ilipopiga zahanati kubwa zaidi ya uzazi Gaza mwezi Disemba, mlipuko huo ulilipua vifuniko kutoka kwenye matenki matano ya maji ya nitrojeni yaliyohifadhiwa katika kitengo cha embriolojia.

Maji hayo ya baridi kali yalipoyeyuka, halijoto ndani ya mitungi hayo ilipanda, na kuharibu zaidi ya viinitete 4,000 pamoja na vielelezo 1,000 vya mbegu za kiume, na mayai ambayo hayajarutubishwa yaliyohifadhiwa katika kituo cha Al Basma IVF huko Gaza.

Viinitete kwenye mizinga hiyo vilikuwa tumaini la mwisho kwa mamia ya wanandoa wa Kipalestina wanaokabiliwa na utasa.

"Tunajua kwa undani maisha haya 5,000, au maisha yanayotarajiwa, yalimaanisha nini kwa wazazi, kwa siku za hivi karibuni au siku zilizopita," alisema Bahaeldeen Ghalayini, 73, daktari wa uzazi aliyefunzwa na Cambridge ambaye alianzisha kliniki hiyo mwaka 1997.

Karibia nusu ya wanandoa - wale ambao hawawezi tena kutoa manii au mayai kutengeneza kiinitete - hawatakuwa na nafasi nyingine ya kupata mimba, alisema.

"Moyo wangu umevunjika vipande vipande," alisema.

Miaka mitatu ya matibabu ya kushika mimba ulimpa msongo wa mawazo Seba Jaafarawi.

Utoaji wa mayai kutoka kwake ulikuwa kwa uchungu, na sindano za homoni alizochomwa zilikuwa na madhara makubwa, alikumbwa na huzuni mkubwa wakati majaribio mawili ya kushika mimba kushindikana awali.

Jaafarawi, 32, na mumewe hawakuweza kupata mimba kwa njia ya kawaida na wakageukia njia ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi (IVF), ambayo inapatikana kwa wingi huko Gaza.

Familia ya idadi kubwa ni jambo la kawaida katika eneo hilo, ambapo karibu nusu ya watu wako chini ya miaka 18, na kiwango cha uzazi ni cha juu, watoto 3.38 kwa kila mwanamke, kulingana na Ofisi ya Takwimu ya Palestina. Kiwango cha uzazi cha Uingereza ni watoto 1.63 kwa kila mwanamke.

Licha ya umaskini Gaza, wanandoa wanaokabiliwa na utasa wanafuata IVF, wengine wakiuza TV na vitu vingine ili walipie huduma hiyo, Al Ghalayini alisema.

Kuna kliniki kama tisa huko Gaza zilifanya IVF, ambapo mayai hukusanywa kutoka kwa mayai ya mwanamke na kurutubishwa na manii kwenye maabara. Mayai yaliyorutubishwa, yanayoitwa viinitete, mara nyingi hugandishwa hadi wakati mwafaka wa kuhamishiwa kwenye uterasi ya mwanamke. Viinitete vingi vilivyogandishwa huko Gaza vilihifadhiwa katika kituo cha Al Basma.

Mnamo Septemba, Jaafarawi alipata uja uzito, jaribio lake la kwanza la IVF lililofanikiwa.

"Sikuwa na muda wa kusherehekea habari hio ya uja uzito," alisema.

"Ningemalizaje ujauzito wangu? Ni nini kingetokea kwangu na wale walio ndani ya tumbo langu?" Alisema hivyo wakati Israeli ilipoanza kushambulia Gaza baada ya kushambuliwa na Hamas Oktoba mwaka jana.

Uchunguzi wa ultrasound yake haikufanyika na Ghalayini alifunga kliniki yake, ambapo viinitete vitano vya ziada vya Jaafarawi vilihifadhiwa.

Mashambulizi ya Waisraeli yalipozidi, Mohammed Ajjour, daktari mkuu wa maswala ya afya ya wanawake wa kituo cha Al Basma, alianza kuwa na wasiwasi kuhusu viwango vya nitrojeni katika tanki tano za sampuli.

Baada ya vita kuanza, Ajjour alifanikiwa kupata usambazaji mmoja wa nitrojeni, lakini Israeli ilikata umeme na mafuta Gaza, huku wasambazaji wengi walifunga kazi.

Oktoba mwishoni, vifaru vya Israeli viliingia Gaza na askari wavamizi walifunga barabara karibu na kituo cha IVF. Ikawa ni hatari sana kwa Ajjour kuangalia hifadhi ya matanki.

Jaafarawi alijua anapaswa kupumzika ili kulinda ujauzito wake dhaifu, lakini hatari zilikuwa kila mahali: alipanda ngazi sita hadi kwenye nyumba yake kwa sababu lifti iliacha kufanya kazi; bomu lilibomoa jengo jirani na kulipua madirisha ya gorofa yake; hivyo chakula na maji kupungua.

Badala ya kupumzika, alikuwa na wasiwasi.

"Niliogopa sana na kulikuwa na dalili kwamba ningepoteza mimba," alisema.

Jaafarawi alivuja damu kidogo baada ya yeye na mumewe kuondoka nyumbani na kuhamia kusini mwa Khan Younis. Damu ilipungua, na hofu yake kuongezeka. '

'Maisha ya 5,000 kwenye ganda moja'

Walivuka hadi Misri mnamo Novemba 12, walipofika mjini Cairo, uchunguzi wa kwanza ulionyesha kuwa alikuwa na ujauzito wa mapacha na walikuwa hai.

Lakini baada ya siku chache, alipata maumivu ya tumbo, kutokwa na damu na mabadiliko ya ghafla katika tumbo lake. Alifika hospitali, lakini alikuwa ashaipoteza mimba.

"Sauti za mimi kupiga kelele na kulia hospitalini bado (zinasikika) masikioni mwangu," alisema.

Bado niko na maumivu ya kupoteza mimba.

"Chochote unachofikiria au ninakuambia juu ya jinsi safari ya IVF ilivyokuwa ngumu, huezi kunifahamu, ni wale tu ambao wamepitia wanajua jinsi ilivyo," alisema.

Jaafarawi alitaka kurudi kwenye eneo la vita, kurudisha viinitete vilivyogandishwa na kujaribu IVF tena.

Lakini alikuwa ashachelewa sana.

Ghalayini alisema kombora moja la Israel liligonga kona ya kituo, na kulipua maabara ya embryolojia ya ghorofa ya chini. Hajui ikiwa shambulio hilo lililenga maabara haswa au la.

"Maisha haya yote yalipotea au kuondolewa: 5,000 wanaishi kwenye ganda moja," alisema.

Mnamo Aprili, maabara ya embryolojia ilikuwa bado imejaa vifusi, vifaa vya maabara vilivyolipuliwa na matangi ya nitrojeni ya kioevu, kulingana na mwandishi wa habari wa Reuters ambaye alitembelea eneo hilo.

Vifuniko vilikuwa wazi na bado vikionekana chini ya moja ya miungi ya gesi, pamoja na kikapu kilichojazwa na mirija midogo yenye viini vilivyoharibika.

Pata Habari Zaidi kupitia WhatsApp channels

CHANZO:TRT World