| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Somalia yasikitishwa na uingizwaji wa silaha kutoka Ethiopia
Serikali ya Somalia imepaza sauti kuhusu uingizwaji haramu wa silaha nchini humo kutoka Ethiopia.
Somalia yasikitishwa na uingizwaji wa silaha kutoka Ethiopia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Ahmed Moallim Fiqi ameuita uingizwaji huo kama mchakato hatarishi kwa amani na usalama wa Somalia./Picha: Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia / Others

Somalia imeonesha wasiwasi wake juu ya uingizwaji haramu wa silaha katika eneo la Pembe ya Afrika, kutoka nchi jirani ya Ethiopia.

Akizungumza jijini Mogadishu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Ahmed Moallim Fiqi ameuita uingizwaji huo kama mchakato hatarishi kwa amani na usalama wa Somalia.

Pia, ameitaka Ethiopia kuheshimu makubaliano, huku akipongeza juhudi za usuluhishi baina ya nchi hizo jirani, uliofanywa na Uturuki.

Taarifa ya awali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia, ilidai kuwa Ethiopia ilisambaza silaha katika eneo la Puntland.

'Malori mawili yaliyosheheni silaha'

Somalia ilidai kuwa inao ushahidi wa malori mawili yaliyowasili Puntland kutoka Ethiopia, yakiwa yamesheheni silaha.

Somalia ilielezea tukio hilo kama "dharau kubwa kwa uhuru wa kujitawala wa Somalia na una hatarisha, sio tu usalama wa nchi, bali wa kanda nzima."

Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye uhasama wa muda sasa.

Hata hivyo, Uturuki imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa nchi hizo zinafikia mapatano.

Umoja wa Mataifa umepongeza jitihada za Uturuki katika kumaliza tofauti kati ya nchi hizo, kupitia mazungumzo yaliyofanyika mwezi Julai na Agosti.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika