| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
DRC: Ajali ya helikopta yaua 3
Helikopta hiyo, ambayo inamilikiwa na Jeshi la Ulinzi la DRC (FARDC) ilipata ajali kwenye uwanja wa ndege wa Ndolo jijini Kinshasa.
DRC: Ajali ya helikopta yaua 3
Watu wapatao watatu walipoteza maisha kwenye ajali hiyo iliyohusisha helikopta ya Jeshi la Ulinzi la DRC./Picha: Agence Congolaise de Presse / Others
30 Oktoba 2024

Watu wapatao watatu wamepoteza maisha kufuatia ajali iliyohusisha helikopta inayomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la DRC (FARDC) jijini Kinshasa siku ya Oktoba 30.

Kulingana na vyanzo vya kijeshi, helikopta hiyo ilipata ajali majira ya asubuhi katika eneo la kurukia la uwanja wa ndege wa Ndolo ulioko jijini Kinshasa.

Abiria wote watatu, akiwemo rubani wa chombo hicho, rubani msaidizi na mhandisi wa helikopta hiyo wamefariki dunia kufuatia ajali hiyo kulingana na vyombo vya habari vya nchi hiyo, vikiongeza kuwa rubani wa helikopta hiyo alibanwa na mkanda wa kiti kwenye helikopta hiyo na kufa papo hapo.

Abiria wengine wawili walifariki dunia wakiwa njiani kufikishwa hospitalini, kulingana na mamlaka ya usalama wa anga ya nchi hiyo (RVA).

Taarifa hizo, pia zilithibitishwa na Jenerali Fae Ngama, kamanda wa FARDC.

Kulingana na Christophe Lomami, meya wa Barumbu, chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika