| Swahili
AFRIKA
1 DK KUSOMA
Jeshi la Polisi Tanzania kuchunguza jaribio la kutekwa kwa mfanyabiashara
Kupitia taarifa yake kwa umma, jeshi hilo limeanza uchunguzi wa tukio la mfanyabiashara aliyenusurika kutekwa jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Jeshi la Polisi Tanzania kuchunguza jaribio la kutekwa kwa mfanyabiashara
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime./Picha: Wengine / Others
13 Novemba 2024

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limeanza uchunguzi wa picha mjongeo iliyosambaa mitandaoni, ikionesha watu wawili wanaojaribu kumkamata na kumuingiza kwa nguvu ndani ya gari mfanyabiashara mmoja jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lililomuhusisha mfanyabiashara huyo aitwaye Deogratius Tarimo, limeripotiwa na yeye mwenyewe katika kituo cha Polisi Gogoni jijini Dar es Salaam, siku ya Novemba 11, 2024.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania David Misime, inasema kuwa kulingana na ushahidi uliowasilishwa kituoni hapo na Tarimo mwenyewe, ni kuwa mfanyabiashara huyo alifika kwenye hoteli iiitwayo Rovenpic iliyopo eneo la Kilivya jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kufanya mazungumzo ya biashara na watu aliokuwa akiwasiliana nao toka Oktoba 25, 2024.

CHANZO:TRT Afrika