| swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Jeju Air aomba radhi kwa ajali ya ndege  Korea Kusini
Katika kikao kifupi na wanahabari, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji Kim E-bae anasema kuwa kuunga mkono wafiwa ni jambo la kipaumbele kwa sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jeju Air aomba radhi kwa ajali ya ndege  Korea Kusini
Wakati huo huo, Boeing ilitoa salamu za rambirambi na kusema inawasiliana na Jeju Air ya Korea Kusini baada ya ajali hiyo mbaya. / Picha: Reuters
29 Desemba 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Korea Kusini Jeju Air amewaomba radhi waathiriwa wa ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya takriban watu 167 Jumapili iliyopita.

Katika kikao kifupi na wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Kim E-bae alisema kuwa kuunga mkono wafiwa ni jambo la kipaumbele kwa sasa.

Wakati huo huo, Boeing ilitoa salamu za rambirambi na kusema inawasiliana na Jeju Air ya Korea Kusini baada ya ajali hiyo mbaya.

Ajali hiyo ilihusisha ndege aina ya Boeing 737-800, kulingana na Jeju Air.

Ndege ya Jeju Air iliyokuwa na watu 181 kutoka Bangkok kuelekea Korea Kusini ilianguka siku ya Jumapili ilipowasili, na kugongana na kizuizi na kuwaka moto, huku watu wawili pekee walionusurika wakiokolewa hadi sasa.

Mgongano na ndege wanaopaa na hali mbaya ya hewa ilitajwa na mamlaka kama sababu zinazowezekana za ajali hiyo iliyowatupa abiria nje ya ndege na kuiacha "karibu kuharibiwa kabisa", kulingana na maafisa wa zima moto.

Video ilionyesha ndege ya Jeju Air ikitua kwa tumbo bila magurudumu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan, ikiserereka kutoka kwenye njia ya ndege huku moshi ukitoka kwenye injini, kabla ya kuangukia ukuta na kulipuka kwa moto.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Trump ailalamikia Katiba ya Marekani kutomruhusu kuwania muhula wa tatu
Israel yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza na kukiuka makubaliano ya kusitisha vita
Malkia wa zamani wa Thailand Sirikit afariki dunia akiwa na umri 93
Maseneta wa Marekani wanamtaka Trump kuchukua msimamo thabiti dhidi ya unyakuzi wa West Bank
Waziri Mkuu wa Israel amfuta kazi msaidizi wake mkuu wa usalama kwa mtafaruku juu ya Gaza
Mbu wapatikana nchini Iceland kwa mara ya kwanza
Kiongozi Mkuu wa Iran, Khamenei, apinga madai kuwa Marekani imeharibu uwezo wa nyuklia wa nchi yake
Mashambulizi mapya ya Israel yawauwa takriban Wapalestina 21 huko Gaza licha ya kusitishwa kwa vita
Gaza inaishutumu Israel kwa wizi wa viungo kutoka kwa Wapalestina, inataka uchunguzi wa kimataifa
ICC inakataa ombi la Israel la kukata rufaa kuhusu vibali vya kukamatwa kwa Netanyahu na Gallant
Israel yapunguza upatikanaji wa misaada kwa nusu, inazuia mafuta kuingia Gaza
Mabomu ambayo hayajalipuka yana hatari 'kubwa' huko Gaza, NGO yaonya
Marekani katika kizungumkuti cha kutumia dhahabu yake kulipia deni la taifa
'Sura mpya kwa amani' — Dunia inajibu baada ya kusaini hati rasmi ya kumaliza vita vya Gaza
Viongozi wa Marekani, Uturuki, Misri, na Qatar wamesaini makubaliano yanayositisha vita vya Gaza
Kuachiliwa kwa mateka kutaanza Gaza saa 11 alfajiri, vyombo vya habari vya Israel vinaripoti
Israel inadhulumu wafungwa Wapalestina kabla ya kuachiliwa chini ya makubaliano na Hamas, video inaonyesha
Trump, Sisi kushirikiana kuandaa mkutano wa Gaza huko Sharm el-Sheikh nchini Misri
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2025
Wapalestina 200,000 wanarejea kaskazini mwa Gaza huku wanajeshi wa Israel wakiondoka