AFRIKA
2 DK KUSOMA
Vijana wanne Kenya waliokuwa wametoweka wamepatikana
Viongozi wa kidini na wa mahakama wameshutumu kupotea kwa vijana hao wakidai kuwa serikali ina jukumu la kuwaachia huru.
Vijana wanne Kenya waliokuwa wametoweka wamepatikana
Billy Mwangi aliripotiwa kupotea tangu Disemba 21, 2024 / Picha: Wengine kupitia X  / Others
6 Januari 2025

Jumatatu asubuhi vijana wanne nchini Kenya ambao wanaodaiwa kutekwa nyara nyara wamejitokeza wakiwa hai.

Familia za Billy Mwangi, Peter Muteti, Bernard Kavuli na Rony Kiplangat wamesema jamaa wao walikuwa wamewasiliana nao. Mwangi na Muteti walikuwa wamekutana na familia zao tayari.

Billy Mwangi aliripotiwa kupotea Disemba 21, 2024.

Rony aliyeripotiwa kupotea Disemba 25, 2024, alipatikana katika Kaunti ya Machakos, na Bernard Kavuli, aliyetekwa nyara Ngong kupatikana Kitale.

Peter Muteti alipatikana katika mji wa Nairobi.

Kijana mwengine Kibet Bull ambaye alipotea baada ya kuchora katuni iliyohusishwa kumkejeli Rais William Ruto, bado hajulikani alipo. Steve Mbisi, ambaye pia ameripotiwa kutoweka bado hajapatikana.

Hata hivyo, kuna ripoti kuwa familia yake imesema imepata ripoti kutoka kwa ndugu yake Rony Kiplangat, ambaye alipotea kabla ya mchora katuni huyo kuripotiwa kutekwa nyara.

CHANZO:TRT Afrika