| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Ouattara wa Ivory Coast autaka tena Urais
Rais Alassane Ouattara anahudumu muhula wake wa tatu licha ya katiba ya nchi hiyo kuruhusu mihula miwili tu kwa marais.
Ouattara wa Ivory Coast autaka tena Urais
Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast./Picha: AFP    / Others
9 Januari 2025

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amesema kuwa angependa kuendelea kusalia madarakani, licha chama chake kutopitisha jina la mgombea kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

Kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 83 alichaguliwa kuongoza kwa muhula wa tatu mwaka 2020, kufuatia kura ya maoni iliyopigwa mwaka 2016, iliyomuongeza muda wa kubakia madarakani.

Katika uchaguzi uliopita, Ouattara alisistiza kuwa alikuwa na baraka zote za kura hiyo ya maoni ili kuendelea kusalia madarakani.

Ikumbukwe kuwa, Outtara alionesha nia ya kuachia madaraka, hata hivyo, alisema kuwa atahitaji upinzani ili kubadili msimamo wake.

"Nina afya njema tu na nina ari ya kuendelea kuiongoza nchi yangu,” alisema Outtara wakati akiwahutubia mabalozi jijini Abidjan.

Mwaka jana, aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Gbagbo, Simone Gbagbo, alitangaza nia yake ya kugombea Urais mwaka 2025.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika