AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kenya inaunga mkono suluhisho la mataifa mawili kati ya  Israeli na Palestina - Rais Ruto
Rais wa Kenya William Ruto amempongeza Rais wa Misri Abdelfattah El-sisi kwa kuhusika kwake katika juhudi za amani nchini Somalia, Sudan na Mashariki ya Kati.
Kenya inaunga mkono suluhisho la mataifa mawili kati ya  Israeli na Palestina - Rais Ruto
Kenya na Misri zimesaini mikataba 12 katika sekta mbalimbali, ikiwemo biashara, uwekezaji, elimu na utafiti, na teknolojia, miongoni mwa mengine. /Picha: @WilliamsRuto X / Others
30 Januari 2025

Na Mustafa Abdulkadir

TRT Afrika / Istanbul

Rais wa Kenya William Ruto amesema nchi yake inaunga mkono suluhisho la mataifa mawili katika mzozo wa Israeli na Palestina na na inakubaliana na azimio nambari 2728 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la 2024, ambalo linataka kusitishwa mara moja kwa mapigano.

Kupitia ukarasa wake wa X, Rais Ruto amesema, “Amejadili na mwenzake wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi, migogoro barani Afrika ambayo imesababisha watu kupoteza maisha, watu kuhama makazi yao na uharibifu wa mali na maisha.

Kwa sababu hii, ni muhimu kwamba tufanye kazi pamoja ili kukomesha mapigano haya, kunyamazisha bunduki na kurejesha amani na utulivu - hasa katika Sudan, Somalia na Mashariki mwa DRC - kwa ajili ya maendeleo endelevu ya bara.”

Vilevile amemshukuru Rais wa Misri kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Somalia, Sudan na Mashariki ya Kati.

Amesema hayo akiwa na Rais wa Misri Abdelfatah El-sisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Cairo.

Kwa upande wake Rais Sisi amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kibiashara na uwekezaji kati ya Misri na Kenya, hasa kwa kuunga mkono uwepo wa makampuni ya Misri katika soko la Kenya.

Nchi hizo mbili zimesaini mikataba 12 katika sekta mbalimbali, ikiwemo biashara, uwekezaji, elimu na utafiti, na teknolojia, miongoni mwa mengine.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika