| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Serikali ya Tanzania yamsaka Mange Kimambi
Mange Kimambi amethibitisha kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwa serikali ya Tanzania imefungua kesi dhidi yake na hivyo kupanga kumrudisha Tanzania.
Serikali ya Tanzania yamsaka Mange Kimambi
Mwanaharakati Mange Kimambi, amelaumiwa na serikali ya Tanzania kwa kuchochea maandamano ya vurugu nchini humo. /@mangekimambi / x
3 Desemba 2025

Mwanaharakati maarufu katika mitandao ya kijamii, Mange Kimambi, anayeishi Marekani, ameshitakiwa kwa kuharibu uchumi nchini Tanzania.

Miongoni mwa mashitaka anayokabiliwa nayo ni utakatishaji wa fedha.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Tanzania, shauri hilo limepangwa kusikilizwa tarehe 4 Disemba, mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Aidha, kesi hiyo iliwasilishwa dhidi ya Kimambi tarehe 28 Agosti, 2025.

Mange Kimambi amethibitisha kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwa serikali ya Tanzania imefungua kesi dhidi yake na hivyo kupanga kumrudisha Tanzania.

Hapo awali Mwanasheria Mkuu wa serikali nchini Tanzania, Hamza Johari, amemlaumu mwanaharakati huyo kwa kuchochea maandamano ya vurugu katika nchi hiyo, na kusema "lazima tumkamate".