| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Ubalozi wa Uturuki unaomboleza kifo cha Mkuu wa Jeshi wa Libya
Ubalozi wa Uturuki nchini Libya umehuzunishwa na kifo cha Mkuu wa Jeshi wa nchi hiyo, Mohammed al-Haddad, ambaye alifariki katika ajali ya ndege pamoja na maafisa kadhaa wakuu wa kijeshi, alipokuwa akirejea kutoka ziara rasmi nchini Uturuki.
Ubalozi wa Uturuki unaomboleza kifo cha Mkuu wa Jeshi wa Libya
Mabaki ya ndege hiyo yalipatikana katika kijiji cha Kesikkavak katika wilaya ya Haymana mjini Ankara. / / AA
24 Desemba 2025

Miongoni mwa waliofariki pamoja na al-Haddad ni Kamanda wa Kikosi cha Ardhini, Brigedia Jenerali na mpiga picha wa ofisi ya vyombo vya habari vya jeshi.

Katika taarifa yake, ubalozi wa Uturuki ulisema kuwa umehuzunishwa sana na vifo hivyo.

"Tunaomba Mungu awarahemu waliofariki na tunatoa rambirambi zetu pamoja na dua za kuwapapa subira kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wananchi wote wa Libya, familia zao na wenzao katika jeshi," ilisema taarifa hiyo.

Mabaki ya ndege binafsi ya Falcon 50 yalipatikana na maafisa wa usalama wa Uturuki katika wilaya ya Haymana karibu na Ankara, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki.

CHANZO:TRT Arabi, TRT Afrika