| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Trump awaamuru makamanda kuandaa mpango wa uvamizi wa Greenland: Ripoti
Maafisa wakuu wa kijeshi wanaripotiwa kupinga mpango wa rais, kulingana na ripoti hiyo.
Trump awaamuru makamanda kuandaa mpango wa uvamizi wa Greenland: Ripoti
Rais Donald Trump anazungumza kwenye mkutano na watendaji wakuu wa mafuta katika Ukumbi wa Mashariki wa Ikulu ya White House, Ijumaa, Januari 9, 2026, huko Washington. / AP
11 Januari 2026

Rais wa Marekani Donald Trump ameagiza makamanda wa vikosi maalum kuandaa mpango wa uvamizi wa Greenland, iliripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.

Washauri wenye msimamo mkali wa sera karibu na Rais wa Marekani, baada ya mafanikio ya Washington katika operesheni ya kijeshi ya Januari 3 huko Venezuela ambayo ilimteka Rais Nicolás Maduro na mkewe, wanataka kusonga haraka ili kuchukua kisiwa hicho kabla Urusi au China yafanye hatua, lilisema gazeti hilo.

Kulingana na ripoti, Trump ameagiza Kamanda wa Operesheni Maalum za Pamoja kuandaa mpango wa uvamizi, lakini viongozi wakuu wa majeshi wanapinga hatua hiyo, wakidai itakuwa kinyume cha sheria na haitaungwa mkono na Bunge la Congress

'Hatutaki kuwa Wamarekani'

Ijumaa, viongozi wa vyama vya siasa vya Greenland walisema, "Hatutaki kuwa Wamarekani, hatutaki kuwa Wadenmaki, tunataka kuwa Wagrinlandi," kufuatia matamshi ya Trump yaliyonyesha nia ya kuchukua Greenland.

Akiwa katika tukio Ikulu Ijumaa, Trump alisema, "Tutafanya kitu kuhusu Greenland, wapende wasipende kwa sababu ikiwa hatutafanya, Urusu au China watachukua Greenland, na hatutaki Urusi au China kama jirani." Aliongeza, "Ningependa kufanya mkataba kwa njia rahisi, lakini kama hatutafanya kwa njia rahisi, tutafanya kwa njia ngumu."

Matamshi ya Trump yamepata lawama, huku nchi za Ulaya hasa zikitahadharisha kwamba hatua kama hiyo inaweza kumaanisha mwisho wa NATO.

CHANZO:TRT Afrika