| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Israel yawahamisha wafanyakazi wake wa ubalozi kutoka UAE
Ndege hiyo iliondoka Dubai na kupewa ruhusa maalumu ya kutua kwenye uwanja wa Ben Gurion, licha ya uwanja huo kutoruhusu ndege za abiria kutua.
Israel yawahamisha wafanyakazi wake wa ubalozi kutoka UAE
Mchakato huo, ulifanyika kupitia operesheni maalumu, kulingana na KAN./Picha:Wengine
tokea masaa 5

Israel ilitumia ndege maalumu kuwasafirisha wafanyakazi wake wa ubalozini kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kuelekea Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion, ulioko jijini Tel Aviv, siku ya Jumanne.

Kulingana na shirika la habari la Israel (KAN), wafanyakazi wa ubalozi wa nchi waliokuwa jijini Abu Dhabi na Dubai, pamoja na familia, na kuwapeleka mapema Jumanne.

Mchakato huo, ulifanyika kupitia operesheni maalumu, kulingana na KAN.

Ndege hiyo iliondoka Dubai na kupewa ruhusa maalumu ya kutua kwenye uwanja wa Ben Gurion, licha ya uwanja huo kutoruhusu ndege za abiria kutua.

Maeneo kadhaa, ikiwemo UAE, pamoja na Kuwait, Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, Oman, Jordan na Iraq, yameripotiwa kuathirika na mashambulizi kutoka Iran, tangu siku ya Jumatatu, kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

CHANZO:AA