| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mufti Mkuu wa Tanzania atoa wito wa utulivu
Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir ameomba umoja na utulivu licha ya maandamano yaliyopangwa kufanyika Disemba 9.
Mufti Mkuu wa Tanzania atoa wito wa utulivu
Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubaka Zubeir, aliwaomba wananchi kuwa na subira na kuruhusu viongozi wa dini waendelee na mazungumzo. / / Wengine
8 Desemba 2025

Mufti Mkuu wa Tanzania amesema ni vyema Watanzania “waache matangazo na kauli zinazochochea chuki” na waweke mikakati ya mazungumzo na maridhiano badala ya machafuko.

Mufti Mkuu pia aliwaomba wananchi kuwa na subira na kuruhusu viongozi wa dini waendelee na mazungumzo.

“Endeleeni kuwa watulivu, kulinda amani, na kuepuka vichochezi vyovyote, iwe mitandaoni au sehemu nyingine yoyote,” aliongeza.

Mufti huyo pia amesema kwamba taasisi za dini nchini zimeanza mazungumzo yenye lengo la kuimarisha amani na kulinda maisha na mali za wananchi.

Katika tamko lake lililotolewa Disemba 7, Mufti Zubeir alisema mazungumzo hayo yanaendeshwa kwa usimamizi wa Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Nuhu Mruma.

“Mazungumzo yameanza kupitia Taasisi ya Tanzania Interfaith Partnership (TIP), ambayo kwa sasa inasogezwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, baada ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kumaliza kipindi chake cha usimamizi,” alisema Mufti Zubeir.

Alisisitiza kuwa viongozi wa dini wana jukumu la kuendeleza amani na heshima ndani ya jamii, na kuwa “tusiruhusu dini au imani ziwe njia ya kuwahamasisha watu kufanya maandamano yanayoweza kuleta mgogoro”.

CHANZO:TRT Afrika