| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mo Dewji azidi kung’ara orodha ya matajiri barani Afrika
Kulingana na jarida la Forbes, Dewji, maarufu kama Mo Dewji, anashika nafasi ya 14 kati ya watu matajiri barani Afrika, akiwa na thamani ya Dola bilioni 2.1.
Mo Dewji azidi kung’ara orodha ya matajiri barani Afrika
Rais wa heshima wa Simba Sports Club na mfanyabiashara Mohammed Dewji./Picha:Wengine
tokea masaa 5

Mfanyabiashara Mohammed Dewji anaendelea kuongoza orodha ya matajiri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, licha ya kushuka kwa nafasi mbili katika orodha ya mabilionea wa Afrika iliyotolewa hivi karibuni.

Kulingana na jarida la Forbes, Dewji, maarufu kama Mo Dewji, anashika nafasi ya 14 kati ya watu matajiri barani Afrika, akiwa na thamani ya Dola bilioni 2.1.

Kwa upande mwingine, rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe, amepanda kwa nafasi moja kwenye orodha hiyo, na kushika nafasi ya 8, huku mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote, akiendelea kuongoza orodha hiyo, baada ya thamani yake kupanda na kufikia Dola bilioni 28.5.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Johann Rupert na familia yake, wakiwa na thamani ya Dola bilioni 16.1, huku Abdulsamad Rabiu akiwa wa tatu, kwa utajiri wenye thamani ya Dola bilioni 11.2.

CHANZO:TRT Afrika Swahili