Uchungu wa familia nchini Kenya wakati mtoto akiwa vitani Ukraine
AFRIKA
3 dk kusoma
Uchungu wa familia nchini Kenya wakati mtoto akiwa vitani UkraineKujifanya ana matatizo ya akili na picha za kuonesha ajali ya kupangwa ndicho kilichomfanya Duncan Chege apate kukimbia kutoka Ukraine.
Jamaa wa raia wa Kenya wanaoaminika kupigana kwa niaba ya Urusi nchini Ukraine wakiwa kwenye maandamano jijini Nairobi. / REUTERS
tokea masaa 12

Na Emmanuel Oduor

Kabla ya kupata majeraha ya mabomu ya kutegwa baharini ambayo yalichana viatu vyake na kufanya mguu uwe na damu, Duncan Chege alikuwa amemtumia mke wake video ya yeye akijificha katika shimo moja chini ya mti kwenye mstari wa mbele nchini Ukraine. 

Video ilikuwa sehemu ya ushahidi kwa familia yake katika kaunti ya Kiambu nchini Kenya kuhusu namna alivyolaghaiwa – kwa ahadi ya kupewa kazi nchini Urusi ya dereva wa lori ambayo ilibadilika kuingizwa kupigana katika vita viya Ukraine vinavyoendelea kwa mwaka wa tano wiki hii.

Mama yake aliiambia TRT Afrika kipindi alichokuwa na wasiwasi kuhusu Chege akiwa Ukraine, huku mtoto wake akituma picha akiwa na magwanda ya kijeshi. Alikuwa ameuza ng’ombe pekee wa familia ili mtoto wake apate nauli ya kwenda Urusi na kupata kukopa watu ili mwanawe aweze kurudi kutoka Urusi.

“Walimdanganya kuhusu kazi lakini nashkuru Mungu mtoto wangu amerudi salama. Maisha yake ni muhimu kwangu kuliko kitu kingine chochote kile,” aliiambia TRT Afrika.

Chege, mwenye umri wa miaka 30 ni baba wa mtoto mmoja, alikuwa hana ajira na alikuwa anaishi na familia yake pamoja na wazazi kabla ya kuondoka. Wakala wa kazi alimuahidi mshahara wa dola $2,500 kila mwezi nchini Urusi.

Safari hiyo ndefu kutoka uwanja wa ndege hadi Moscow iliishia katika kambi ya jeshi ya Urusi, akapewa mafunzo ya wiki moja, alafu kupelekwa katika kambi ya jeshi nchini Ukraine.

Chege anakadiria kuwa idadi ni sawa na ile iliotajwa na Shirika la Ujasusi la Kenya wiki iliopita kwa bunge kuwa huenda ikawa kuna raia wa Kenya zaidi ya 1,000 ambao wanapigania Urusi dhidi ya Ukraine.

“Kuna Waafriika wengi ambao wanapigana nchini Ukraine, na wengine wengi wameuawa. Nimeona miili yao tukiwa vitani,” alikiambia chombo cha habari cha Kenya.

Serikali kote barani Afrika zimewahi kuonya raia wao dhidi ya kujiunga kwenye vita hivyo. Mataifa mengine kama Kenya na Afrika Kusini wameitaka Urusi kusaidia kurudisha miili ya raia wao na wale waliokamatwa kama wafungwa wa kivita.

Mapema mwezi huu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi alitangaza kuwa atasafiri hadi Moscow kwa mazungumzo yanayolenga "kupata suluhu ya suala hilo na kubaini suluhu endelevu".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa wii hii alitembelea Ukraine na kumuomba Rais Volodymyr Zelensky kuwaachilia wafungwa wawili wa Ghana waliokamatwa wakipigania Urusi.

Wakiwa kwenye kambi ya pili ya kijeshi nchini Ukraine, Chege na wenzake, kama anavyowaita yeye, walipewa mafunzo ya mwezi mmoja kuhusu matumizi ya mabomu, kabla ya kupelekwa kwenye "maeneo hatari".

Alielezea chombo hicho cha habari cha Kenya kuhusu namna walivyokuwa katika kijiji kimoja cha Ukraine, waliona miili imetapakaa pembeni mwa barabara, akikadiria huenda idadi huenda ikawa ni mamia. Wanajeshi waliojeruhiwa hawakupata usaidizi wa kimatibabu, alisema, akieleza kuhusu matukio hatari ya wanajeshi waliopasuliwa matumbo na wengine waliokatwa viungo.

Kujifanya ana matatizo ya akili na picha za kupanga ajali zilizotumwa na mke wake ndizo zilizomfanya Chege akimbie kutoka Ukraine.

“Hilo likamfanya daktari amruhusu kwenda kwa kamanda, na hapo ndipo nilipoenda ubalozi wa Kenya na kufanikiwa kusafiri hadi nyumbani” alilimbia shirika hilo la habari.

CHANZO:TRT Afrika English
Soma zaidi
Afrika Kusini yabaini zaidi ya wafanyakazi hewa 4,000 miongoni mwa wafanyakazi wa serikali
Papa Leo XIV kuzuru nchi ya Cameroon, Angola, Algeria na Guinea ya Ikweta
DRC yaanzisha mashambulizi dhidi ya M23 katika maeneo kadhaa
Ukraine yatoa onyo kwa raia wa Ghana kutojiunga na majeshi ya Urusi
Tanzania yatoa tahadhari ya ongezeko la maambukizi ya mafua, Uviko 19 na Dengue
Mwanasiasa wa Zambia mbaroni kwa 'picha iliyobadilishwa kidijitali' ya Rais Hichilema
Baraza la Usalama la UN limewawekea vikwazo makamanda wanne wa RSF kwa ukatili wa Al Fasher
Takriban watu milioni 6.5 nchini Somalia wanakabiliwa na njaa kali kutokana na ukame, UN yasema
Cameroon yasema kifo cha mwanasiasa wa upinzani aliyekamatwa Anicet Ekane "ni cha asili"
Tinubu amteua mkuu wa polisi mpya katikati ya vitisho vinavyoongezeka vya usalama nchini Nigeria
Moto katika uwanja wa ndege wa Cape Town nchini Afrika Kusini wasitisha safari kadhaa
Msemaji wa M23, Willy Ngoma, auawa katika shambulio la droni mashariki mwa DRC
Uharibifu mkubwa Chuo Kikuu cha Kordofan Sudan baada ya shambulizi la anga la RSF
Afrika Kusini kubatilisha viza 2,000 zilizopatikana kwa njia isiyo sahihi baaada ya uchunguzi
Rais Sisi wa Misri awasili Saudi Arabia kwa 'ziara ya kindugu'
Mpaka wa Burundi na DRC wafunguliwa tena baada ya kufungwa kwa miezi miwili
Somalia yapongeza uhusiano unaokua kati yake na Uturuki
Kufunga saum kwa wagonjwa wa Kisukari: Njiapanda kati ya Imani na usalama wa afya
AU inataka kuchukuliwa kwa 'hatua za pamoja' baada ya watu zaidi ya arobaini kuuawa nchini Nigeria
Tume ya Rais kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi Tanzania yaongezewa siku 42 kuhitimisha uchunguzi