| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Watu 22 wapoteza maisha, 16 kujeruhiwa baada ya majengo kuporomoka nchini Morocco
Waendesha mashitaka nchini humo, wametoa amri ya kuanza kwa uchunguzi wa kubaini chanzo cha tukio hilo.
Watu 22 wapoteza maisha, 16 kujeruhiwa baada ya majengo kuporomoka nchini Morocco
Kulingana na chombo cha habari cha eneo hilo, majengo hayo yenye ghorofa mbili kila moja, yaliporomoka katika eneo la Fes./Picha:Wengine
10 Desemba 2025

Watu wapatao 22 wamepoteza maisha na wengine 16 kujeruhiwa kufuatia tukio la kuporomoka kwa majengo mawili ya makazi, kaskazini mwa Morocco, siku ya Jumatano.

Kulingana na chombo cha habari cha eneo hilo, majengo hayo yenye ghorofa mbili kila moja, yaliporomoka katika eneo la Al-Massira kitongoji cha Fes.

Chombo cha habari cha serikali ya Morocco 2M kimesema kuwa vikosi vya uokoaji vilikuwa eneo la tukio vikiendelea kutafuta manusura wa tukio hilo.

Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuhusu chanzo cha tukio hilo.

Majeruhi wa tukio hilo waliwahishwa mahospitalini, huku wakazi wa maeneo jirani wakihamishwa kutoka kwenye nyumba zao.

Waendesha mashitaka nchini humo, wametoa amri ya kuanza kwa uchunguzi wa kubaini chanzo cha tukio hilo.

CHANZO:AA