tokea masaa 7
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha mkataba wa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleiman ‘Morocco’.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Novemba 4, 2025 na shirikisho hilo, mkataba huo umesitishwa kwa makubaliano ya pande mbili, yaani TFF kwa upande mmoja na Kocha Morocco kwa upande mwingine.
Kutokana na hatua hiyo, TFF imemteua Kocha Miguel Gamondi wa timu ya Singida Black Stars kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars.
Rais huyo wa Argentina anatarajiwa kuiongoza Taifa Stars kwenye Fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Morocco, kuanzia Disemba 2025.








