Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na mwenzake kutoka Finland Alexander Stubb, wamejadiliana mahusiano ya nchi zao, masuala ya kikanda na ya ulimwengu kupitia mazungumzo ya simu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Rais Erdogan alisisitiza nia ya Uturuki kukuza kiwango cha biashara na Helsinki.
Kulingana na Rais Erdogan, Uturuki inazingatia umalizwaji wa mchakato wa amani kati ya Ukraine na Urusi, akiongeza kuwa mazungumzo ya Istanbul yataonesha ufanisi katika hilo.
"Rais Erdogan aligusia kuwa Uturuki inafuatilia kwa ukaribu mkataba wa wa usitishwaji mapigano huko Gaza, na kwamba amani ya kudumu inaweza kupatikana kupitia suluhu ya dola mbili, na kuwa Uturuki itapongeza uamuzi wa Finland wa kulitambua taifa la Palestina," ilisema Kurugenzi hiyo.
Rais Erdogan alitumia fursa hiyo kumpongeza rais wa Finland kwa sherehe za siku ya uhuru wa nchi hiyo, zitakazofanyika Disemba 6.



















