UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki yatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika mji wa Al Fasher, Sudan
Ankara pia imetoa wito wa kuhakikisha upitishaji salama wa misaada ya kibinadamu bila vizuizi vyovyote na kusitisha mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia.
Uturuki yatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika mji wa Al Fasher, Sudan
Vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la Sudan na RSF vilivyoanza tangu Aprili 2023 bado vinaendelea. / / AA
tokea masaa 11

Uturuki imetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigani katika mji wa Al Fasher nchini Sudan na maeneo yanayoizunguka.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imesisitiza umuhimu wa kuhakikisha upitishaji salama kwa misaada ya kibinadamu, kuondoa vikwazo vinavyokwamisha utoaji wake, na kumaliza mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia.

Wizara hiyo ilisema kuwa Ankara inafuatilia kwa wasiwasi mkubwa yanayojiri hivi karibuni nchini Sudan na inakubaliana na taarifa iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusu suala hilo.

Wizara hiyo imelaani vikali ukatili uliofanywa dhidi ya raia katika mji wa Al Fasher.

Mji wa Al Fasher umedhibitiwa na wanamgambo wa RSF mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wizara hiyo pia imesisitiza msimamo thabiti wa Uturuki wa kuunga mkono, uhuru wa mipaka, na mamlaka ya Sudan, ikibainisha umuhimu wa mazungumzo ili kupata suluhisho la amani kwa mgogoro huo.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la Sudan na RSF vimeanza tangu Aprili 2023, na vimesababisha vifo vya maelfu ya watu huku zaidi ya watu milioni 14 wakilazimika kuhama makazi yao kutokana na mapigano hayo.

CHANZO:AA