| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Denmark yamtimua mwanadiplomasia wa Urusi baada ya jaribio la kumuua rapa wa Ukraine
Akizungumzia uamuzi huo, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alisema uamuzi unalenga kuonesha umakini wa nchi kwenye masuala yanayohusu Denmark na bara la Ulaya kwa ujumla.
Denmark yamtimua mwanadiplomasia wa Urusi baada ya jaribio la kumuua rapa wa Ukraine
Akizungumzia uamuzi huo, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alisema uamuzi unalenga kuonesha umakini wa nchi kwenye masuala yanayohusu Denmark. / Others
 

Waziri wa Mambo ya Nje ya Denmark, Lars Lokke Rasmussen ametangaza kumfukuza nchini humo, afisa ulinzi ndani ya Ubalozi wa Urusi jijini Copenhagen, baada ya kubainika kuhusika na jaribio la kutaka kumuua rapa wa Ukraine.

"Tumemwita balozi wa Urusi wizarani na kumjulisha uamuzi wetu wa kumfukuza afisa wao anayeshughulika na ulinzi, awe ameondoka nchini kwetu ndani ya siku saba,” alisema Rasmussen.

Waziri huyo, aliongeza kuwa, Denmark ilikuwa kwenye mchakato wa kusitisha utoaji wa visa za Schengen kwa raia wa Urusi.

Akizungumzia uamuzi huo, Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alisema uamuzi unalenga kuonesha umakini wa nchi kwenye masuala yanayohusu Denmark na bara la Ulaya kwa ujumla.

Mapema Ijumaa, idara ya kijasusi ya Denmark (PET), ilisema ilishuku mpango wa Urusi wa kutaka kumuua msanii wa Ukraine, wakati wa tamasha lililofanyika jijini Copenhagen, kwa msaada wa kikundi cha kihalifu cha Denmark kilichopigwa marufuku tangu mwaka 2021.

CHANZO:AFP