Maoni
AFRIKA
3 dk kusoma
Kiswahili, siyo Kifaransa, ndiyo lugha sahihi Afrika Mashariki
Lugha ndiyo roho ya watu. Kukipa thamani Kifaransa kuliko Kiswahili Afrika Mashariki kunafanya utambulisho wa utamaduni kudunishwa pamoja na uhusiano wa kikanda.
Kiswahili, siyo Kifaransa, ndiyo lugha sahihi Afrika Mashariki
Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu milioni 200 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. / Wengine
6 Oktoba 2025

Katika taifa ambalo watu wanazungumza lugha nyingi kama Uganda, ambapo kuna lugha zaidi ya 40 zinazungumzwa kote nchini, ni wazi kuwa ni njia ambayo lugha inaweza kuimarisha au kudumaza mafanikio.

Mgombea urais Mubarak Munyagwa amezua taharuki kwa kupendekeza kuondoa lugha ya Kiswahili katika orodha ya lugha za taifa na badala yake kutumia lugha ya Kifaransa.

Ahadi yake, ikiwa ni hatua ya kwenda na wakati, inapuuza utamaduni na kudharau urithi wa Uganda na nafasi yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kwa Uganda, Swahili siyo lugha tu; ni njia ya kuleta mafanikio ya kiuchumi na amani, na kufanya pendekezo la kutumia Kifaransa kuwa lisilo na msingi.

Kiuchumi, Kiswahili hakiwezi kubadilishwa na chochote. Uganda, ni nchi ambayo kimkakati uchumi wake unakuwa Afrika Mashariki, na imejumuishwa vizuri, ikiwemo Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Lugha inayotumika katika kanda

Kiswahili ni lugha ambayo inatumika sana, inazungumzwa na watu zaidi ya milioni 200 kote katika kanda. Ni lugha ambayo inatumika katika masoko ya Nairobi, makubaliano ya kidiplomasia mjini Arusha, na biashara kutoka nchi moja hadi nyingine ambayo inasaidia kusafirisha kahawa ya Uganda, dhahabu, na bidhaa za kilimo.

Ufahamu wa lugha ya Kiswahili hausaidii katika kuchagiza biashara tu; inafungua uwekezaji, utalii, na ajira.

Juhudi za Uganda kufanya Kiswahili kuwa somo shuleni tangu 1992, zinadhihirisha hili.

Uganda ni koloni la zamani la Uingereza, siyo Ufaransa; Kiingereza tayari kinatumika zaidi ulimwenguni. Kulazimisha raia wa Uganda kuzungumza Kifaransa kutawafanya watengwe, kwa kuwafanya wajifunze lugha ambayo inawaweka mbali na shughuli zao za kila siku na majirani zao.

Kiswahili, lugha ambayo asili yake ni lugha za Kibantu kinazungumzwa na mamilioni ya watu nchini Uganda—kutoka lugha ya Luganda hadi Runyankole.

Siyo sadfa kwamba Kiswahili ni lugha pendwa katika wilaya ya Uganda kama vile Kiryandongo, ambapo kinatumika zaidi, au katika maeneo ya mipakani kama vile Bwera, ambapo kinazungumzwa kwa ufasaha.

Roho ya watu

Pendekezo la Munyagwa siyo tu haliwezekani; ni kurudisha watu nyuma zaidi. Uganda imekuwa ikipambana kuzungumza Kiswahili vizuri kulingana na uhusiano wa kihistoria na utawala uliopita, lakini katika mabadiliko ya hivi karibuni ya mitaala kumekuwa na matumaini.

Kuachana na Kiswahili sasa hivi kutafanya maendeleo ya miongo mingi kuonekana kama hayana faida, kutengwa kwa taifa, na kudumaza kukuwa kwa uchumi.

Ingekuwa bora watunga sera wakatumia raslimali zao kuwapa mafunzo walimu na kuhamasisha vyombo vya habari kuimarisha ufasaha wa Kiswahili.

Kama ambavyo Waziri Mkuu Robinah Nabbanja alivyothibitisha, Kiswahili “ni muhimu sana katika kuleta umoja Afrika Mashariki.”

Kwa kumalizia, lugha siyo jambo la kuchezewa—ni roho ya watu. Kwa kukipa Kifaransa kipaumbele kuliko Kiswahili, Munyagwa anaiweka hatarini Uganda na Afrika Mashariki.

Ni usaliti wa utamaduni wetu, majirani zetu, na mustakabali wetu. Uganda inahitaji viongozi ambao wana lengo la kuimarisha lugha —na lugha hiyo ni Kiswahili, siyo Kifaransa.

Mwandishi, Isaac Bagaya ni mhadhiri wa Kiswahili nchini Uganda.

Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitizamo na sera ya uhariri ya TRT Afrika.


CHANZO:TRT Afrika