Umoja wa Mataifa Jumatatu umesema kuwa Israel imefunga mipaka yote ya kuingia Gaza na kusitisha uwasilishaji wa misaada ya kibinadamu ndani na karibu na maeneo ambayo vikosi vya Israel vinaendelea kuyakalia.
"Mamlaka ya Israel imefuga mipaka yote, ikiwemo Rafah, na imesitisha uingizaji wa misaada ya kibinadamu ndani na karibu na maeneo ambayo vikosi vya Israel vinaendelea kuwepo Gaza. Pia wamesitisha mzunguko wa wafanyakazi wetu wa masuala ya kibinadamu," msemaji wa UN Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari .
"Watu Gaza, kama unavyojua, wanategemea misaada ya kibinadamu kutoka nje. Kutokana na uwezo mdogo wa kuhifadhi na uharibifu uliofanyika katika eneo la vita, sisi na washirika wetu tumejaribu kuendelea na uwasilishaji wa misaada licha ya kuendelea kuwepo kwa vikwazo, lakini hiyo haiwezi kuendelea kunapokuwa na vikwazo kamili," amesema.
"Ni muhimu kwa mipaka yote kufunguliwa haraka iwezekanavyo," amesema.
Katika eneo la West Bank linalokaliwa, Dujarric amesema vikosi vya Israel vimefungwa sehemu nyingi za ukaguzi, kuzuia shughuli zote kati ya miji ya Palestina na majimbo.
"Sheria ya kimataifa ya kibinadamu iko wazi. Kama tunavyosema kila siku na mara nyingi, mara nyingi kwa siku, raia sharti walindwe na wapate mahitaji yao ya lazima, ikiwemo kutembea na kupata misaada ya kibinadamu," amesema.
Jumamosi asubuhi, Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran, kwa madai kwamba ilitaka kuondoa "tishio" la "utawala" wa Iran. Katika majibu, Iran iliilenga Israel na kambi za Marekani zilizopo katika eneo hilo.
Israel imetanga "hali ya hatari" nchi nzima.










