| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Majeshi ya Israel yazingira ‘Kaburi la Yosefu’
Tukio hilo, ni mwendelezo wa uvamizi wa majeshi ya Israel, kwenye maeneo mbalimbali matakatifu, ambayo ulianza Septemba 26.
Majeshi ya Israel yazingira ‘Kaburi la Yosefu’
Tukio hilo, ni mwendelezo wa uvamizi wa majeshi ya Israel, kwenye maeneo mbalimbali matakatifu, ambayo uliaanza Septemba 26.

Raia wa Israel, wakisaidiwa na wanajeshi wa nchi hiyo, mapema Alhamisi walivamia na kuzingira eneo linaloaminika kuwa kaburi la Yosefu, mashariki mwa jiji la Nablus.

Kulingana na Shirika la Habari la Palestina (WAFA), wanajeshi hao, walivamia eneo hilo na kuwaamuru wakazi wa hapo, kuondoka mara moja.

Muda mfupi baadaye, eneo hilo liligeuzwa kuwa kambi kijeshi, ambapo walenga-shabaha walijificha juu ya majengo mbalimbali, wakitoa ulinzi kwa raia wa Israel, waliokuwa wakishiriki ibada ya Kitalmudic.

Tukio hilo, ni mwendelezo wa uvamizi wa majeshi ya Israel, kwenye maeneo mbalimbali matakatifu, ambao ulianza Septemba 26.

Siku ya Jumatano, Waisraeli wapatao 2,500 walivamia msikiti wa Al-Aqsa mashariki mwa Yerusalem, wakiwa wanalindwa na wanajeshi wa Kiisrael.

Tangu watwae eneo la Ukingo wa Magharibi mwaka 1967, waumini wa Kiyahudi wanalichukua eneo hilo kama sehemu takatifu, wakiamini ndipo yalipo maziko ya Yosefu, mwana wa Yakobo.

CHANZO:Anadolu Agency