| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Marais Paul Kagame, Felix Tshisekedi watia saini mkataba wa kumaliza machafuko mashariki mwa DRC
Utiaji saini wa mkataba huo wa amani unakuja miezi mitano, baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na DRC kukutana na Rais Trump, na kuonesha nia yao ya kumaliza mapigano.
Marais Paul Kagame, Felix Tshisekedi watia saini mkataba wa kumaliza machafuko mashariki mwa DRC
Mkataba huo, maarufu kama ‘The Washington Accord’, ulisainiwa nchini Marekani Disemba 4, 2025./Picha:Reuters
tokea masaa 17

Rais Donald Trump wa Marekani aliwaongoza Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa DRC kwenye kutiliana saini mkataba amani wenye kulenga kumaliza machafuko katika eneo la Mashariki mwa DRC.

Mkataba huo, maarufu kama ‘The Washington Accord’, ulisainiwa nchini Marekani Disemba 4, 2025.

"Itakuwa ni muujiza mkubwa, " alisema Trump mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.

Akiwazungumzia viongozi hao wawili kutoka Afrika Mashariki, Trump alisema: "Walitumia muda mrefu kuuana, ila kwa sasa watatumia muda wao kufurahi pamoja, hususani wakifaidi matunda ya kiuchumi ya Marekani."

Hata hivyo, viongozi hao walikuwa na kauli tofauti kidogo mara baada ya kutia saini mkataba huo.

"Ni wazi kuwa haitokuwa rahisi huko tuendako,” alisema Kagame.

Kwa upande wake, Rais Tshisekedi aliuita mkataba huo kama “mwanzo mpya”.

Fursa ya madini

Kulingana na Trump, mkataba huo utatoa fursa kwa Marekani kuanza kuchimba madini adimu yanayopatikana DRC na Rwanda.

"Tutaanza kuchimba madini hayo adimu, na kila mtu atapata pesa nyingi,” alisema Trump.

Utiaji saini wa mkataba huo wa amani unakuja miezi mitano, baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na DRC kukutana na Rais Trump, na kuonesha nia yao ya kumaliza mapigano.