| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yashitakiwa Mahakama ya Afrika Mashariki kwa kuzima Intaneti
Kupitia shauri hilo, wanaharakati uzimwaji wa intaneti nchini Tanzania ulikuwa na athari kwenye uchumi, jamii na haki za kiraia.
Tanzania yashitakiwa Mahakama ya Afrika Mashariki kwa kuzima Intaneti
Mitandao ya kijamii ilizimwa nchini Tanzania, siku moja baada ya maandamano yaliyotatiza shughuli za uchaguzi mkuu nchini humo./Picha:@RoseAchana
tokea masaa 2

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) kimefungua kesi katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), kupinga uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzima huduma za intaneti, kati ya Oktoba 29 na Novemba 4, 2025 nchini humo.

Katika shauri lao, watetezi hao wa haki za kibinadamu, wanadai kuwa uamuzi huo ulikwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo ambao pia ulikandamiza haki za msingi za raia.

Waliopo ‘kikaangoni’ katika kesi hiyo, ni pamoja na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini humo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na baadhi ya makampuni ya simu nchini humo.

Walalamikaji hao wanataka uamuzi huo uharimishwe, kuwepo na zuio la maamuzi kama hayo siku zijazo, na kuwepo msahama wa wazi kufuatia tukio hilo.

Kupitia shauri hilo, wanaharakati uzimwaji wa intaneti nchini Tanzania ulikuwa na athari kwenye uchumi, jamii na haki za kiraia.

Wakati huo huo, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) wameishitaki serikali ya nchi hiyo katika mahakama ya EACJ, wakipinga zuio la siku tano la kutotoka nje, lililotekelezwa jijini Dar es Salaam.

 

 

CHANZO:TRT Swahili