| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania: Bado kuna akiba ya kutosha ya mafuta
Hali hiyo inatokana na uwepo wa akiba ya kutosha ya mafuta katika taifa hilo la Afrika Mashariki ambayo inaweza kukidhi mahitaji kwa miezi kadhaa ijayo.
Tanzania: Bado kuna akiba ya kutosha ya mafuta
Mussa Mohammed Makame, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). / TRT Afrika Swahili
tokea masaa 2

Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa hali ya mgogoro inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati haitarajiwi kusababisha ongezeko la bei ya mafuta ya ndege wala gharama za usafiri wa anga kwa sasa.

Hali hiyo inatokana na uwepo wa akiba ya kutosha ya mafuta nchini ambayo inaweza kukidhi mahitaji kwa miezi kadhaa ijayo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Mohammed Makame, ambae amesema kuwa hadi sasa hakuna dalili za athari kubwa katika sekta ya anga nchini kutokana na mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa serikali, mafuta yanayotumika kwa sasa yaliagizwa tangu mwezi Januari na bado yapo katika kiwango kinachokidhi mahitaji ya ndani ya nchi.

Vilevile imebainishwa kuwa hadi sasa vita vinavyoendelea katika eneo hilo havijaathiri kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa mafuta wala shughuli za sekta ya usafiri wa anga nchini.

Serikali imeeleza kuwa inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa soko la kimataifa ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati unaendelea kuwa wa uhakika na gharama za usafiri zinabaki kuwa nafuu kwa watumiaji.