Afrika
Jeshi la Sudan ladhibiti Ikulu ya Rais jijini Khartoum
Uhasama kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya kikosi cha RSF umeanza mwezi Aprili 2023.
21 Machi 2025

Jeshi la Sudan latangaza kuchukua tena Ikulu ya Rais huko Khartoum, ikulu hiyo ni ngome ya mwisho iliokuwa ikidhibitiwa na kikosi cha RSF kinachoongozwa na  Mohammed Hamdan Dagalo.

Aidha, video na picha zimesambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha wanajeshi wa Sudan wakiwa ndani ya Ikulu kama ishara ya udhibiti huo.

Vita ndani ya jiji la Khartoum vimekua vikiendelea kwa kasi baada ya jeshi kuweza kuchukua udhibiti wa jimbo la Aljazeera na miji iliyokuwa karibu na Khartoum.

Uhasama kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya kikosi cha RSF umeanza mwezi Aprili 2023, na kusababisha mgogoro mkubwa Sudan, huku watu wengi wakilazimshwa kuyahama makazi yao.

Tazama Video zaidi
Mgombea wa Zanzibar: Ali Hassan Mwinyi
Uchaguzi Tanzania na ahadi Lukuki
Zitto ataka Kigoma iongoze kwa kila kitu
Mgombea Urais Tanzania aahidi kufuga mamba Ikulu
Luhaga Joelson Mpina: Panda shuka yake ya siasa ya Tanzania hadi upinzani
Afrika yajadili mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano nchini Ethiopia
Uganda kupokea wahamiaji kutoka USA
Mpina: Sirudi CCM ng'oo
Chama cha upinzania Tanzania NLD chataka fursa sawa kuelekea Uchaguzi Mkuu
CHAUMMA yaahidi mageuzi ya uchumi