| swahili
00:40
Afrika
Kura zinaendelea kuhesabiwa Tanzania
30 Oktoba 2025

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, lakini hili linafanyika huku kukiwa na hofu kutokana na miji mikubwa haina watu barabarani baada ya polisi kukabiliana na waandamanaji.

Dar es Salaam, ambalo ni jiji la kibiashara limetatizika zaidi baada ya polisi kutangaza amri ya kutotoka majumbani kuanzia saa kumi na mbili jioni. Hii ni baada ya waandamanaji kujitokeza barabarani na baadhi yao kuharibu majengo ikiwemo kuchoma moto kituo cha polisi.


Kutokana na hali hii maeneo mengi ya biashara yamefungwa huku polisi na jeshi wakionekana wakishika doria au kuwepo katika baadhi ya sehemu. Nchi pia imekumbwa na kusitishwa kwa intaneti kote, jambo lililotatiza utoaji huduma ikiwemo kutumia usafiri wa umma.

Watumishi wa umma wameagizwa kufanyia kazi kutoka majumbani.

Tazama Video zaidi
Rais Samia atangazwa mshindi
Mwinyi ashinda uchaguzi Zanzibar
Ulinzi mkali jijini Dar es Salaam kufuatia Uchaguzi Mkuu
Raia wa Tanzania waanza kupiga kura
Kampeni zakamilika Tanzania
'Coco Beach': Maisha yanasonga kawaida
Kasi ya biashara yapungua jijini Dar es Salaam Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Tanzania: Wito wa amani watolewa kwa Uchaguzi Mkuu 2025
Uchaguzi Tanzania 2025: Je, unafahamu haya kuhusu uchaguzi mkuu?
Safari ya Urais ya Raila Odinga