8 Septemba 2025
Viongozi wa Afrika wanakutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa katika mkutano wao wa pili wa mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika.
Ni mpango mkakati wa bara unaolenga kuzisaidia nchi za Afrika kupata ufumbuzi wa baadhi ya changamoto katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, changamoto wanazodai kuwa haziwezi kupuuzwa tena.