1 Septemba 2025
Chama tawala nchini Tanzania, CCM kimezindua kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani, wabunge na Urais.
Kampeni hizo zilizinduliwa kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, ambako chama hicho kilimnadi mgombea wake Samia Suluhu Hassan.
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, unatarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.