| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Burhan amfuta kazi mpinzani wake aliyekua makamu
Jenerali Abdel Fattah al Burhan amemteua aliyekuwa kiongozi wa waasi Malik Agar kuwa naibu wake kuchukua nafasi ya Mohamed Hamdan Dagalo.
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Burhan amfuta kazi mpinzani wake aliyekua makamu
Takriban watu 705 wameuawa katika mzozo huo, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni Picha: Reuters / Others
19 Mei 2023

Kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al Burhan amemfuta kazi makamu wake na kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) Mohamed Hamdan Dagalo.

Wawili hao walihudumu kama mwenyekiti na naibu wa Baraza Kuu linalotawala baada ya mapinduzi ya kijeshi mnamo Oktoba 2021.

Lakini mvutano kati yao ulizuka na kuwa vita ambavyo havijawahi kushuhudiwa mwezi Aprili kwa ajili ya udhibiti wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali lenye zaidi ya watu milioni 46.

Takriban watu 705 wameuawa katika mzozo huo, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni.

Katika agizo la Ijumaa, Jenerali Burhan alimteua aliyekuwa kiongozi wa waasi Malik Agar kuwa naibu wake kuchukua nafasi ya Dagalo.

Aliagiza mamlaka husika kutekeleza agizo hilo mara moja.

Kufukuzwa huko kuna uwezekano wa kuathiri uwanja wa vita ambapo pande zinazozozana zinaonekana ziko kwenye mkwamo na kutotaka kumaliza uhasama, shirika la habari la AP linaripoti.

CHANZO:TRT Afrika