AFRIKA
2 DK KUSOMA
Uchaguzi DRC 2023: CENI kuanza kutoa matokea ya awali
Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, iliongeza muda wa kupiga kura katika baadhi ya maeneo hadi jana Alhamisi.
Uchaguzi DRC 2023: CENI kuanza kutoa matokea ya awali
Raia wa DRC pia walipiga kura kwenye nchi tano Canada, Marekani, Ufaransa, Ubelgiji na Afrika kusini. / Picha: Reuters
22 Desemba 2023

Akizungumza kwenye mojawapo ya vituo vya redio DRC, afisa wa ngazi ya juu wa Tume ya Uchaguzi CENI, Didi Manara alisema kuwa Tume ya Uchaguzi itaanza kuchapisha matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais siku ya Ijumaa.

Baadhi ya maeneo kama vile mji mkuu wa Kinshasa, tayari yameanza kushuhudia matokeo yaliyochapishwa nje ya vituo vya kupiga kura.

Wananchi wa DRC wamepiga kura kuchagua rais, wabunge wa kitaifa na kikanda pamoja na madiwani wa mitaa.

Mnamo siku ya Alhamisi, Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, iliongeza muda wa kupiga kura katika baadhi ya maeneo.

Rais wa sasa Felix Tshisekedi, ambaye alichukua madaraka mwaka 2019, anawania kiti hicho kwa muhula mwengine wa pili.

Wagombea 18 wa upinzani pia wanawania urais nchini humo.

CHANZO:AFP