| Swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Biden: Mauaji ya kiongozi wa Hamas hayatosaidia hatua za kumaliza vita
Mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza yameingia siku ya 301, yakiwa yameua Wapalestina 39,480, wengi wakiwa wanawake na watoto na kujeruhi wengine 91,128 na wengine zaidi ya 10,000 wakiwa wamefukiwa kwenye vifusi.
Biden: Mauaji ya kiongozi wa Hamas hayatosaidia hatua za kumaliza vita
Wakazi wa eneo la Gaza wanahofia kuwa mauaji ya Haniyeh yataongeza vita zaidi. / Picha: AA   / Others

Rais wa Marekani Joe Biden amesema mauaji ya kiongozi wa kikundi cha Kipalestina cha Hamas Ismail Haniyeh hakijsaidia kumaliza vita vya Israeli dhidi ya Gaza.

Kumekuwa na hatari ya kuongezeka kwa vita vya Mashariki ya Kati baada ya mauaji ya Haniyeh nchini Iran yalisababisha vitisho vya kulipiza kisasi dhidi ya Israeli.

Kikundi cha Hamas na kile cha kimapinduzi vilithibitisha kifo cha Haniyeh, ambaye alishiriki kwenye mazungumzo ya kumaliza vita katika eneo la Gaza.

"Hayatosaidia lolote," Biden aliwaambia wanahabari baada ya kuulizwa iwapo mauaji ya Haniyeh yatazorotesha mazungumzo ya amani.

Biden pia alisema alikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu mapema Alhamisi.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika